Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afrika Kusini yaaga Kombe la Dunia ikichapwa jioooni

Muktasari:

  • Kwa kufunga bao hilo, Eustaquio anakuwa mchezaji wa tatu anayecheza Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kufunga bao katika hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Dunia.

Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ imeaga fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji wenza, Canada kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa SoFi, Marekani.

Aliyekatisha ndoto za Afrika Kusini kufika hatua za majuu za mashindano hayo ni Stephen Eustaquio aliyeifungia Canada bao hilo pekee la ushindi katika dakika za majeruhi za mchezo.

Mchezo ulionekana kama ungefika katika dakika 30 za nyongeza na hata mikwaju ya penalti kutokana na uimara mkubwa wa safu ya ulinzi ya Afrika Kusini kuokoa mashambulizi ya Canada.

Hata hivyo, Eustaquio aliihakikishia ushindi Canada kwa bao ambalo alifunga kwa shuti la mguu wa kulia mpira aliounasa baada ya kuokolewa kwa kichwa na beki wa Afrika Kusini, Mbekezeli Mbokazi.

Kwa kufunga bao hilo, Eustaquio anakuwa mchezaji wa tatu anayecheza Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kufunga bao katika hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Dunia.

Kabla yake waliowahi kufanya hivyo walikuwa ni Landon Donovan na Brian McBride.

Afrika Kusini inakuwa timu ya pili ya Afrika kuaga mashindano hayo ikifuata nyayo za Tunisia ambayo iliishia hatua ya makundi.

Canada sasa inamsubiri mshindi wa mchezo baina ya Uholanzi na Morocco ambaye itakutana naye katika hatua ya 16 bora.