Wanaotaka kujichora mwili waombe ushauri wa daktari

Madaktari na wataalamu wa afya wanadai baadhi ya watu kuharibu miili na afya zao kwa ushabiki au kwa kutojua na kuaswa kabla ya maamuzi ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu, vinginevyo madhara yake yanaweza kuwa majuto.
Imezoeleka kuwaona watu wakivuta sigara hadharani na wengine wakiwa wamejichora tatoo katika miili yao na kuendelea na majukumu, ila wataalamu wa afya wanadai vitu hivyo vina madhara kiafya na hivyo kutakiwa kuviepuka au kupata ushauri wa daktari kabla ya maamuzi.
Kwa mujibu wa wanasayansi wa afya ya jamii, michoro inayotokana na rangi za madukani pamoja na vichoreo vyake vinaweza kusababisha magonjwa, ikiwemo homa ya uti wa mgongo, tatizo la macho pamoja kansa ya mfumo wa haja ndogo (mkojo) kwa madai kuwa vifaa hivyo hutumika kwa zaidi ya mtu mmoja.
Licha kuwa Totoo inatajwa kuwa ni moja ya pambo katika mwili ila wanasayansi wanadai iko na madhara mengi miongoni mwao ni kansa ya ngozi, makovu, damu kuganda pamoja na majuto itakapobainika kufanyika uamuzi ambao haukuwa sahihi.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC News, Machi, 2020 unadai kufanya utafiti na kugundua ugonjwa wa mapafu, saratani, matatizo ya moyo na kiharusi husababishwa na uchafuzi wa hewa chafu na kunasibishwa na uvutaji sigara na kudai kupata takwimu za vifo vya watu zaidi 8.8 milioni wakiwemo wanaotumia uraibu wa sigara.
Pia kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuna zaidi ya kemikali 4,000 katika moshi wa sigara na 50 kati yake zinatajwa kuwa chanzo cha saratani ikiwemo pia madhara katika mfumo wa kupumua na mapafu.
Machi mwaka 2021, Serikali kupitia kwa Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii, wakati huo, Dr, Seif Rashid, alipiga marufuku uvutaji sigara katika maeneo ya umma ili kulinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
Wataalamu wa afya vile vile wanadai kuvuta sigara moja kwa siku upo uwezekanao wa asilimia 50 zaidi kupata magonjwa ya moyo na asilimia 30 kupatwa na kiharusi na kufafanua kuwa wanaume wanaovuta sigara wako na asilimia 48 kupata ugonjwa wa moyo ambapo wanawake wako asilimia 57 ugonjwa huo na asilimia 31 kiharusi.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) watu milioni 8 hufariki kila mwaka kutokana na matumizi ya tumbaku na mamilioni ya wengine wanaishi na magonjwa yanayosababishwa na tumbaku ikiwemo pumu na kifua kikuu.
Licha kuwa viongozi wa dini na baadhi ya wazee kukemea uvutaji sigara na kueleza madhara yake bado jamii hasa kundi la vijana, hivyo ni vyema katazo lililowekwa na aliekuwa Waziri wa Afya wakati huo, Dr, Seif Rashid lizingatiwe ili kupunguza idadi ya watu wanaougua magonjwa yasiyoambukiza.
Baadhi ya watu wanadai licha kampeni nyingi za kupiga vita matumizi ya sigara wakiwemo viongozi wa dini lakini bado hazijafanikiwa kuzaa matunda na hii ni kutokana na kukosekana kwa sheria ambayo itakomesha matumizi hayo.
Mwaka 2007, Tanzania ambayo ni mwanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ilisaini mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku (WHOFCTC) ulioainisha hatua za kisheria na wajibu wa nchi wanachama kukabiliana na tatizo la uvutaji sigara.
Wako baadhi ya watu kuvuta sigara kwenye mikusanyiko ya watu ilhali wanatambua kuwa moshi wa sigara uko na madhara, kwa namna hiyo ni vyema Serikali kupitia watendaji kata kuweka tangazo la onyo uvutaji sigara mbele za hadhara ikiwemo vituo vya mabasi na daladala.
Inaelezwa kuwepo kwa takwimu ionyeshayo asilimia 14.1 ya Watanzania wanavuta sigara kila siku na kulingana na takwimu za Serikali, asilimia kubwa ya maradhi yasiyoambukiza husababishwa na matumizi ya sigara.
Wako wauzaji wa tumbaku mitaani na kudaiwa kuchanganya na aina ya tumbaku itokayo katika sigara inayotajwa kuwa ukitumia uwezekano wa kupata kichefuchefu na kuumwa na tumbo ni rahisi.
Inadaiwa vijana wengi wakiwemo wenye umri wa kwenda shule kushawishika na uraibu wa aina kama hiyo na hii ni kutokana na upatikanaji wake kuwa rahisi.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari na kudai kuwa Serikali imekuwa katika jitihada zinazoendelea ili kupata njia mwafaka kwa kupunguza uzalishaji tumbaku na kuwa na mbadala wa zao hilo ili kulinda afya za wananchi.