Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzizi, suluhu ya changamoto za usimamizi wa mali za familia

Rasilimali ni mali zinazoweza kutumika kuleta tija ya kiuchumi, kama vile ardhi, fedha, habari, ubunifu na watu. Katika kaya, rasilimali zinaweza kuwa nyumba, shamba la kilimo au fedha, ambazo hutumika kuhakikisha ustawi wa familia.

Kwa mfano, kaya inaweza kutumia ardhi yao kwa kilimo ili kupata chakula na mapato.

Katika biashara ndogondogo, rasilimali ni vifaa vya uzalishaji, fedha, watumishi au mfumo wa habari wa biashara, kama vile biashara ya teknolojia inavyotumia ubunifu wake wa programu kama rasilimali kuongeza mapato.

Kati ya matatizo yanayozikumba kaya nyingi na biashara za wajasiriamali wadogo na wa kati ni uelewa, na usimamizi mzuri wa rasilimali.

Kuna fikra kuwa hakuna rasilimali za kutosha kwenye kaya au kwa wafanyabiashara, lakini fikra hii inaweza isiwe sahihi kama kuna usimamizi wa kutosha na endelevu wa rasilimali zilizo ndani ya miliki ya kaya ama biashara hizo.

Changamoto za usimamizi wa rasilimali zinaweza kuwa:

Mosi, kutokuwa na uelewa wa rasilimali: Kaya na biashara nyingi hazina uelewa wa kutosha kuhusiana na rasilimali na namna ya kutumia rasilimali hizo kujiongezea kipato au faida.

Mathalani, kaya inaweza kuwa na ardhi kubwa na ambayo haina tija kwenye uzalishaji, au kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija, na pengine wanakaya hawajiendelezi au kutafuta maarifa ya kuleta tija kwenye ardhi au mifugo yao.

Biashara zinaweza kuleta manufaa makubwa kama kutakuwa na tija kwenye uzalishaji, uuzaji au kuvutia wateja na wanaweza kutokuwa na uwezo wa kuajiri au kujiendeleza ili kuhakikisha biashara inaleta tija inayotakiwa.

Pili, Kipato cha Fedha: Familia na biashara ndogondogo mara nyingi hupata shida katika kukabiliana na mahitaji yao ya kipato cha fedha. Kwa mfano, biashara ndogondogo hupata shida katika kupata mkopo au mtaji wa kukuza biashara zao.

Hii inaweza kusababisha kutokuwa na mtaji wa kutosha, ambapo mauzo ya biashara yanakuwa hayatoshi kulipia gharama za mali na uendeshaji, ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi na kubakiwa na faida.

Tatu, Usimamizi wa watumishi au wanakaya: Katika biashara ndogondogo, usimamizi wa watumishi ni changamoto kubwa. Kwa kiwango fulani, biashara hizi hazina idara ya rasilimali watu rasmi na hivyo kuwafanya wafanyakazi kutokujua majukumu na mipaka ya kazi.

Hii inaweza kusababisha changamoto kama vile kushindwa kuhifadhi wafanyakazi bora au kushughulikia migogoro ya kazi. Kwenye kaya mgawanyo wa kazi za kaya kama haueleweki unafanya wanakaya wasiwe na msukumo kwenye shughuli za kiuchumi za kaya.

Nne, Ulinzi wa rasilimali: Ni muhimu kuweka ulinzi wa rasilimali kutoka madhara kama vile matukio ya tabia ya asili au shida za kiuchumi. Kujikinga na madhara inatakiwa kuwe na mazoea ya kujiwekea bima.

Na tano, ni Uwekezaji wa Rasilimali: Kuweka rasilimali katika mapato yanayotoa faida ni muhimu sana, lakini pia inahitaji ujuzi wa kifedha ambao unakosekana kwenye kaya nyingine na kwa wafanyabiashara ndogondogo.

Hii inaweza kusababisha uamuzi mbaya wa uwekezaji, kama vile kuweka fedha katika miradi isiyo na tija na pia kuwekeza zaidi ya uwezo wa uzalishaji wa rasilimali.

Fuatilia makala zinazofuata kuhusiana na namna bora ya usimamizi wa rasilimali na namna ambayo inaweza kuleta tija kwa biashara ama kwenye kaya.