Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kula na kushiba siyo kwamba umemaliza njaa

Muktasari:

  • Watu wanadhani kula na kushiba ndiyo kumaliza njaa, lakini wanasahau kuangalia aina ya chakula wanachokula kama kinakidhi viwango vya virutubisho vinavyotakiwa mwilini.

Waswahili wanasema mwili haujengwi kwa matofali, bali kwa chakula. Msemo huu una ukweli ndani yake, japo unatakiwa kudadavuliwa kuhusu chakula anachopaswa kula mtu kwa siku.

Watu wanadhani kula na kushiba ndiyo kumaliza njaa, lakini wanasahau kuangalia aina ya chakula wanachokula kama kinakidhi viwango vya virutubisho vinavyotakiwa mwilini.

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) inaonyesha kuwa Serikali hupoteza Sh800 bilioni kwa mwaka sawa na asilimia 2.7 ya Pato la Taifa (GDP) kutokana na madhara ya upungufu wa virutubisho vya chakula kama madini ya chuma, vitamin A na tindikali ya foliki.

Jambo la kwanza la kuelewa ni kuhusu mlo kamili anaotakiwa kupata mtu kwa siku. Mtu anahesabiwa kuwa ameshiba kama atapata mlo kamili wenye mchanganyiko wa vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini na madini kila siku.

Kutopata mlo kamili husababisha mtu kukumbwa na maradhi na mwisho wake ni utapiamlo au mtu kupata kitambi.

Kwa mfano, upungufu wa madini ya chuma husababisha watoto kuwa na mtindio wa ubongo na madini hayo husaidia kuongeza damu mwilini. Ukosefu wa vitamin A husababisha upofu kwa watoto na vifo. Vilevile, ukosefu wa folate (tindikali ya foliki na vitamin B9) husababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Ukosefu wa zinki hupunguza kinga ya mwili na kuongeza uwezekano wa maradhi ya kuhara hasa kwa watoto. Kuna virutubisho muhimu mwilini ambavyo japo vinahitajika kwa kiasi kidogo (micro or milligrams), lakini vikikosekana husababisha madhara makubwa ambavyo ni pamoja na zinc, folate, Niacin (B3), Cobalamin (B12), Thiamine (B1), Ribofalvin (B2), Pyrodoxine (B6) na Selenium. Kwa ujumla, mtu anapaswa kupata miligramu 18 za chuma, miligramu 11 za zinki na gramu 0.15 za iodine katika mlo wake wa siku. Watu wengi hawali vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kama nyama, samaki, kuku, mayai, maziwa, matunda na mbogamboga. Hata ulaji wa vyakula vya mafuta ni mdogo. Mafuta husaidia ufyonzaji wa virutubisho mwilini.

Kutokula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kumesababisha asilimia 34 ya watoto wa Tanzania kudumaa na asilimia 14 kuwa na uzito mdogo kwa mwaka. Vilevile asilimia 17 ya watu wazima hushindwa kufanya kazi za uzalishaji mali kutokana na lishe duni. Madhara mengine ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa neva za fahamu, matatizo ya uzazi, mfumo wa akili na utendaji kazi, ukuaji hafifu na mwisho kuwa mbilikimo, goita, matatizo ya kusikia na kuwa bubu. Binafsi naona zipo njia nyingi za kupambana na upungufu wa virutubisho kama tunavyoelezwa na wataalamu. Wanasema njia hizo ni pamoja na kuongeza virutubisho na uimarishaji wa virutubisho na kuongeza virutubisho kwa njia za kilimo. Kwa mfano, hivi sasa, wataalamu nchini wameshazalisha mbegu za viazi lishe zilizoongezwa virutubisho muhimu mwilini. Viazi hivyo vya rangi ya chungwa huupatia mwili kiasi kikubwa cha vitamin A ukilinganisha na viazi vingine. Kiazi cha gramu 200 kina vitamin A mara tatu zaidi ya kiasi kinachopendekezwa kwa siku. Umuhimu wake ni kuboresha ufanyaji kazi wa macho, ngozi na kukua kwa mifupa, mfumo wa uzazi, tumbo, upumuaji na ukuaji wa mwili. Pia, hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu, huongeza kinga ya mwili, husaidia watu wasizeeke mapema na vina kiasi kikubwa cha vitamin E, B na C, ambazo ni muhimu mwilini. Mbali na kuwa na wanga kwa wingi, viazi hivyo vina vitamin A, C, B1, B2, B3, B5, BC na vitamin K. Vina madini ya chuma, potashamu, manganese kalisiamu, sodiam na folate na protein ambavyo vyote hivi ni muhimu mwilini.

Hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania sasa ajenge utamaduni wa kula chakula bora na watendaji wenye kuhimiza ulaji mzuri waendelee kutoa elimu kwa umma ili kuepuka madhara ya ulaji mbaya kwa jamii.

0754 897 287