Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Semu ateuliwa uenyekiti TCD, Wasira makamu

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Stephen Wasira wakiwa wameshika katiba ya TCD.

Muktasari:

  • Semu ameteuliwa leo Ijumaa Aprili 17, 2026 katika ofisi za TCD zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu amekabidhiwa uenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) atakaohudumu kwa muda mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Katiba ya TCD, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimekabidhiwa nafasi ya umakamu uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Stephen Wasira ameteuliwa kushika nafasi hiyo.

Semu ameteuliwa leo Ijumaa Aprili 17, 2026 katika ofisi za TCD zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

ACT Wazalendo, chini ya Semu kinachukua kijiti hicho, baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumaliza muda wake wa uongozi.

Akizungumza baada ya kuchukua jukumu hilo, Semu amesema katika kipindi chake atajikita kuimarisha maridhiano na ushirikiano miongoni mwa wadau wa siasa.

“Lengo ni kuhakikisha Tanzania inaendelea kujenga demokrasia ya kweli, inabaki kuwa nchi yenye amani, na kutumia amani hiyo kama nyenzo ya kujenga uchumi jumuishi. Hili ni jukumu la Watanzania wote na tunaendelea kulitekeleza,” amesema Semu.

TCD imekuwa na utaratibu wa uongozi wa uenyekiti wa kupokezana kwa vyama wanachama kwa mfumo wa alfabeti.

Kituo hicho kina wanachama wa vyama vya siasa vya ACT Wazalendo, CUF, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) na NCCR-Mageuzi.