Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnyika: Chadema iko katikati vita kubwa dhidi ya watawala

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho kiko katikati ya vita dhidi ya watawala, akidai kuna njama za kupinga uamuzi halali ya vikao vya chama na kujaribu kudhoofisha harakati za kudai mabadiliko ya kisiasa nchini.

Akizungumza leo Ijumaa, Mei 23, 2025, katika kikao maalumu chenye ajenda 12 kinachofanyika Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni-Dar es Salaam, Mnyika amesema wakati huu ni wa kihistoria kwa chama hicho na Taifa, huku akikielezea kikao hicho kuwa sehemu ya kutafakari mustakabali wa Chadema na demokrasia nchini.

“Chama kinapitia wakati mgumu. Tupo katikati ya vita kubwa ya ‘No reforms, no election’ dhidi ya watawala ambao wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi,” amesema Mnyika.

Amedai kuwa Serikali imekuwa ikipinga maamuzi halali ya Baraza Kuu la Chadema lililofanyika Januari 22, 2025, ambalo liliidhinisha uteuzi wa Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wajumbe wa Kamati Kuu.

“Watawala wanafanya kila jitihada kubatilisha maamuzi ya Kamati Kuu ambayo yalifanyika baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Hii ni vita ya wazi dhidi ya chama chetu,” ameongeza.