Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchinjita ajitosa kuomba ridhaa kugomea ubunge ACT Wazalendo

Makamu Mwenyekiti Bara Isihaka Mchinjita akionesha fomu ya kugombea ubunge kwa tiketi ya ACT - Wazalendo leo. Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Mchinjiti anakuwa kada wa kwanza kuomba ridhaa ya kuomba kugombea nafasi ya ubunge kwa Jimbo la Lindi mjini.

Lindi. Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kugombea nafasi ya ubunge Jmbo la Lindi Mjini.

Amesema nia yake ya kuomba ridhaa kwa chama chake ni kutaka kuhakikisha anapigania heshima ya chama na thamani ya kura ya kila Mtanzania na hatamaye ACT Wazalendo ikamate dola.

Mchinjita ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 23, 2025, katika ofisi za ACT Wazalendo zilizopo Lindi Mjini baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na

Katibu wa Jimbo la Lindi Mjini wa ACT Wazalendo, Ahmed Zubery.

Amesema dhamira yake ya kulipambania jimbo na chama kwa ujumla ni kutaka kuona CCM inang’oka jimboni humo.

“Nitahakikisha chama changu kinapambana kwa ujasiri mkubwa kama alivyokuwa Kinjekitile Ngwale alipokabiliana na wakoloni licha ya vitisho na hofu waliyojaribu kueneza, lakini alishinda,” amesema Mchinjita.

Katibu wa Jimbo Lindi Mjini Ahmad Zuberi kutoka kulia akimkabidhi Makamu Mwenyekiti Isihaka Mchinjita fomu ya kugombea ubunge kupitia chama cha ACT- Wazalendo. Picha na Bahati Mwatesa

Katika hatua nyingine, kada huyo wa ACT Wazalendo amesema hatua ya kususia uchaguzi ni sawa na kuikubali hali ya ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Bila kukitaja chama kipi kilichosusia uchaguzi, Mchinjita amesema; "Sitaki kuona tunaendelea kuishi katika zama ambazo tunashuhudia ukandamizaji mkubwa wa kidemokrasia, mauaji, utekaji na upoteaji wa wakosoaji wa Serikali."

Nao baadhi ya Wanachama wa ACT Wazalendo mkoani Lindi wameonyesha imani na matumaini makubwa kwa Mchinjita, wakiahidi kumuunga mkono katika harakati zake za kisiasa.

Bakari Saidi, mmoja wa wanachama hao, amesema Jimbo la Lindi kwa muda mrefu limekuwa ngome ya upinzani kabla ya kupokwa na CCM.

Hata hivyo amesema chake na makada sambamba na wafuasi wa ACT Wazalendo watahakikisha wanalirejesha mikoni mwa chama hicho ili kuendelea na harakati za maendeleo.

"Jimbo la Lindi toka miaka iliyopita lilikuwa ngome ya upinzani, na ndiyo maana tunamuunga mkono Mchinjita ili jimbo hili lirejee mikononi mwa upinzani," amesema Saidi.

Naye Mwajuma Mtambalile alimesema hatua ya Mchinjita kuchukua fomu ya kuomba ridha ndani ya chama ni nzuri na inahitaji kuungwa mkono na kila mwana ACT Wazalendo.

"Tutashirikiana naye kwa hali na mali kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mkuu, kwa kuwa Mchinjita ni kiongozi hodari, mchapakazi, na mwenye kujali maslahi ya wananchi wake," amesema Mtambalile.

Hata hivyo hii ni hatua ya awali ya utoaji wa fomu kwa ngazi ya vyama na Mchinjita ndiye aliyefungua dimba.