Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Nchimbi kuzuru wilaya tano mkoani Mara

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi ameanza ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mara.

Bunda. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi anatarajia kuanza ziara ya siku sita mkoani Mara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020/25.

Katika ziara hiyo, Dk Nchimbi na baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho, watatembelea wilaya zote tano za mkoa huo, ambazo ni Bunda, Rorya, Butiama, Serengeti na Tarime.

Ziara hiyo, inakuja ikiwa ni wiki mbili tangu mtendaji mkuu huyo wa CCM, azuru Mkoa wa Ruvuma, ambako ndiko iliko asili yake.

Maelekezo kwa Serikali, ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2020/25 na kukagua uhai wa chama hicho ngazi ya chini ni miongoni mwa mambo ambayo Dk Nchimbi huyafanya katika ziara zake.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM, Dk Nchimbi ambaye pia ni mgombea mwenza mteule wa urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu,  ataanza ziara hiyo kwa kupokelewa wilayani Bunda leo Jumanne Aprili 22, 2025.

Baadaye jioni atakwenda wilayani Musoma kwa ajili ya kuendelea na ziara hiyo Aprili 23, kisha Butiama Aprili 24.

Dk Nchimbi pia atazuru wilaya ya Rorya Aprili 25, 2025 na ataihitimisha ziara hiyo katika Wilaya ya Serengeti.