Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Nchimbi amrithi Chongolo CCM

Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.

Dar es Saalam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake mpya.

Dk Nchimbi anachukua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu kwa madai ya kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Uteuzi wa Dk Nchimbi umefanyika leo Jumatatu Januari 15, 2024 wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kisha kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyofanyika mjini Unguja, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo Dk Nchimbi alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kukalia kiti hicho kutokana na uzoefu wake kwenye siasa ndani ya CCM na hata serikalini.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii na gazeti la Mwananchi toleo la Januari 16,2024.