Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipukizi CCM walia kudharauliwa

Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa anayemaliza muda wake, Yusuph Kashmir Hajji akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM  (UVCCM) Taifa, Mohammed Kawaida katika mkutano mkuu wa tisa wa chipukizi unaoendelea jijini Dodoma. Picha na Mainda Mhando

Muktasari:

  •  Mwenyekiti anayemaliza muda wake ataka viongozi watakaochaguliwa kuwa wavumilivu na kutokubali kudhalilishwa.

Dodoma. Mwenyekiti wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), anayemaliza muda wake, Yusuph Kashmir Hajji amesema wanakumbana na changamoto ya kudharauliwa.

Ameyasema hayo leo Desemba 20,2023 katika mkutano mkuu wa tisa wa Chipukizi Taifa  unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wakuu unaoendelea jijini Dodoma.

Mkutano huo utawachagua mwenyekiti wa Chipukizi, makamu, wajumbe baraza na mkutano mkuu na kamati ya uendeshaji Taifa.

Kutokana na changamoto hiyo, amewataka viongozi watakaochaguliwa kuwa wavumilivu na kutokubali kudhalilishwa.

"Naondoka lakini niseme tu chipukizi ina changamoto ya kudhalilishwa, ukiwa mwenyekiti hata kama ni wa tawi utapitia changamoto kubwa ikiwa ni  dharau.

Yusuph aliyechaguliwa mwaka 2019 amesema alikuwa na kipindi kigumu cha uongozi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Jokate Mwegelo amezitaka jumuiya za vijana kuheshimiana kila mmoja kwenye nafasi yake, badala ya  kudharauliana.

"Vijana wenzangu tuheshimiane kila mmoja kwa nafasi yake, tupendane, tusaidiane kwa dhati ya mioyo yetu, tuna kazi kubwa ya kumsaidia Rais kwa hiyo tusipoteze muda. Tutumieni muda wetu kupanga mikakati ya chama ili Watanzania waendelee kukiamini chama chetu," amesema.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Mohammed Kawaida amewataka wajumbe watakaopiga kura kuchagua viongozi watakaoenda kuwawakilisha vyema chipukizi.

Kawaida amewapongeza makatibu wa hamasa wa mikoa na wilaya kwa kufanya kazi kubwa kwenye chaguzi za viongozi wa mikoa na wilaya, kwa kuwa kuna maeneo ambayo uchaguzi huo ulirudiwa.