Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yatoa kauli wanaochangiwa fedha za fomu za uchaguzi mkuu

Katibu wa Siasa na Uwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile (kushoto) akiwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa (kulia) wakiashiria uzinduzi wa M-koba ya Chama Cha Wafanyabiashara Soko la Old Airport jijini Mbeya.

Muktasari:

  • Dk Tulia ni Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa bunge la Tanzania, amechangiwa Sh1 milioni kwa ajili ya gharama za uchukuaji fomu ndani ya CCM, kazi inayoanza Juni 28 hadi Julai 2, mwaka huu.

Mbeya. Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya kimesema hatua ya wananchi kuchangia kwa hiari fedha kwa ajili ya kuwasaidia makada wa chama hicho kujiandaa kuchukua fomu za kugombea katika Uchaguzi Mkuu, ni ishara kuwa kazi inayofanywa na chama inaungwa mkono na jamii.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Chama cha Wafanyabiashara wa Soko la Old Airport jijini Mbeya, kumchangia Sh1 milioni Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson ili zisaidie gharama za kuchukua fomu ndani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kwa sasa, CCM imeshatangaza ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa nafasi za Udiwani, Ubunge na Uwakilishi, uchukuaji  utaanza Juni 28 hadi Julai 2, 2025 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza Leo Jumatano Aprili 23, 2025 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi za Chama cha Wafanyabiashara wa Soko la Old Airport, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Mbeya, Christopher Uhagile amesema wananchi kuchangia kwa hiari ni dalili kuwa wana imani na chama hicho.

Ameongeza kuwa kipindi hiki cha uchukuaji na urejeshaji fomu kinawapa fursa wananchi kutathmini na kuchagua viongozi wanaoendana na mahitaji yao.

“Nimesikia baadhi ya wanachama mmeanza kuwachangia fedha wagombea kwa ajili ya kuchukua fomu, sisi kama chama tunapongeza hatua hiyo kwa sababu inaonesha kuwa wananchi wanaridhishwa na kazi ya CCM na viongozi wake, ndio maana Dk Tulia anasema bado yupo imara,” amesema Uhagile.

Amesema dira ya CCM chini ya Mwenyekiti wao, Samia Suluhu Hassan inalenga kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, jambo linaloonekana kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.

Aidha, amewasihi wananchi kuendeleza amani na utulivu, huku akiwapongeza viongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa jitihada zao za maendeleo na kulinda usalama, tofauti na hali iliyokuwepo miaka ya nyuma.

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa, amesema mkoa huo umepiga hatua kubwa kimaendeleo, hususan katika sekta ya elimu.

“Lakini pia tumeweza kujenga zahanati, vituo vya afya, hospitali na kukarabati zaidi ya shule 400 za msingi na sekondari. Pia tumepata maendeleo ya miundombinu kama barabara ya njia nne na mradi mkubwa wa maji kutoka Mto Kiwira,” amesema Meya huyo.

Amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na uongozi wa serikali ya CCM chini ya Rais Samia, na mchango mkubwa wa Dk Tulia kwa wananchi wa Mbeya Mjini, hususan wale wenye uhitaji mkubwa.

Naye Katibu Msaidizi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Soko la Old Airport, Vaileth Simchimba amesema tangu chama chao kianzishwe mwaka 2021, kumekuwa na mafanikio ikiwemo kuongezeka kwa wanachama kutoka 20 na sasa wamefikia 240.

“Tunalenga kusaidiana kiuchumi, lakini tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi. Ili kufanikisha ujenzi wa ofisi na kuendesha shughuli zetu, tunahitaji zaidi ya Sh100 milioni 100,” amesema Vaileth.