Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM, ACT kimeeleweka Zanzibar, SUK rasmi Julai 9

Muktasari:

  • Hatua hiyo inatajwa kuwa muhimu kwa ajili ya kuimarisha maridhiano, mshikamano, utulivu wa kisiasa, amani na ustawi wa Zanzibar.

Dar es Salaam. Baada ya miezi minane ya mazungumzo ya kusaka mwafaka, ni rasmi Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo, keshokutwa Alhamisi, Julai 9, 2026, vitatoa tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa Zanzibar.

Hatua hiyo inatajwa kuwa muhimu kwa ajili ya kuimarisha maridhiano, mshikamano, utulivu wa kisiasa, amani na ustawi wa Zanzibar.

Uamuzi wa kutoa tamko la pamoja umebarikiwa na vikao vikuu vya vyama hivyo, vilivyofanyika kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Julai 7, 2026, na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu ya Zanzibar, Raqey Mohamed, imeeleza kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kushuhudia hafla itakayofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa mbali na Dk Mwinyi, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, atakuwepo wakati wa uwasilishaji huo wa tamko la pamoja na kushuhudia utiaji saini wa ajenda zilizokubaliwa baina ya pande mbili ili kufanyiwa kazi.

“Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini,” imeeleza taarifa hiyo.

Wengine ni wawakilishi wa taasisi za kiraia na waandishi wa habari, na shughuli hiyo itarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuanzia saa nne.

Mazungumzo ya kutafuta mwafaka Zanzibar, yaliyotawaliwa na vuta nikuvute, yalianza Novemba mwaka 2025 yakisimamiwa na Amani Abeid Karume na Dk Ali Mohamed Shein (marais wastaafu wa Zanzibar) kwa upande wa CCM.

Wakati ACT Wazalendo waliwakilishwa na Juma Duni Haji (Mwenyekiti mstaafu wa ACT Wazalendo) na Othman Masoud Othman (Mwenyekiti wa ACT Wazalendo).