Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

App za kujifunza Kiingereza kwa urahisi

Muktasari:

  • Babbel imejikita zaidi kwenye misamiati ikiweka mkazo kwenye ubora wa mafunzo ya lugha unayoyapata kuliko wingi. Kupitia app hii utajifunza kujitambulisha kwa usahihi mbele za watu na kuhakikisha unaweza kuzungumza kiingereza kizuri mbele za watu bila kuishiwa misamiati.
  • Kwa mzazi ambaye anataka mtoto wake tangu akiwa mdogo ajifunze lugha ya Kiingereza, Rosetta stone ndiyo app ya kupakua. Hii itampa mwongozo na kumjengea msingi imara wa kujifunza lugha hiyo. Ataanza kufundishwa namna ya kutamka maneno ya awali na maana zake.

Unaweza ukawa unaumiza kichwa ni namna gani unaweza kujifunza lugha ya Kiingereza ili uweze kuandika na kuzungumza vyema. Kulingana na hali ya utandawazi iliyopo sasa ni muhimu kufahamu lugha zaidi ya moja ikiwemo kiingereza ambayo inatumika zaidi katika soko la kimataifa na ajira.

Wapo wanaokwenda kwenye kozi maalum za lugha hii na wengine wanawatafuta watu waliobobea kuwafundisha katika muda wa ziada. Kwa kuwa sasa teknolojia imerahisha mambo hata lugha hii unaweza kujifunza mwenyewe.

Sasa ukiwa na simu ya kisasa ya mkononi au kompyuta mpakato, unaweza kupakua ‘app’ mbalimbali zinazokuwezesha kuijua vyema lugha ya kiingereza.

Miongoni mwa App hizo ni Duolingo, hii inatajwa kuwa bora zaidi katika ufundishaji wa lugha ya Kiingereza, mwanafunzi anayetumia program hii ana uhakika wa kujifunza lugha ya Kiingereza kwa haraka zaidi.

Wanafunzi wanaipenda zaidi kwa kuwa mfumo wake wa kufundisha umetengenezwa kwa mtindo wa michezo(games) hivyo kuwarahishia kuelewa ndani ya muda mfupi. Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 200 milioni wanatumia program hii kujifunza lugha ya kiingereza na misamiati. Duolingo ni msaada pia kwa walimu kwani inawapa mwongozo wa lugha.

App nyingine ni Busuu, hii inashauriwa zaidi kutumika kwa watu wanaonza kujifunza lugha ya kiingereza. Mtiririko wa mafunzo yake umepangwa kuanzia kwa wale wanaoanza kujifunza hadi ngazi ya watu ambao wanataka kupanua wigo wa uelewa wao.

Kupitia program hii mwanafunzi atafanya mazoezi mbalimbali ya lugha na kila anapomaliza moja anajaziwa matokeo yake kuonyesha namna anavyoelewa. Pia anayo fursa ya kujipima uelewa wake kwa kuomba maswali ya haraharaka ili ayajibu ndani ya muda mfupi.

Kwa wanaotaka kubobea katika majadiliano yanayotumia lugha ya Kiingereza, Babbel ndiyo chaguo sahihi. App hii imesheheni stadi zitakazokuwezesha kumudu kuongea kwa muda mrefu bila kuishiwa misamiati.

Babbel imejikita zaidi kwenye misamiati ikiweka mkazo kwenye ubora wa mafunzo ya lugha unayoyapata kuliko wingi. Kupitia app hii utajifunza kujitambulisha kwa usahihi mbele za watu na kuhakikisha unaweza kuzungumza kiingereza kizuri mbele za watu bila kuishiwa misamiati.

Kwa mzazi ambaye anataka mtoto wake tangu akiwa mdogo ajifunze lugha ya Kiingereza, Rosetta stone ndiyo app ya kupakua. Hii itampa mwongozo na kumjengea msingi imara wa kujifunza lugha hiyo. Ataanza kufundishwa namna ya kutamka maneno ya awali na maana zake.

Ndani ya program hii maneno na mafundisho yapo kwa mfumo wa sauti. Yapo mafunzo mengine ambayo mtaalam anaonekana moja kwa moja akifundisha jambo ambalo linamrahisishia anayejifunza kuelewa kwa haraka.

Awabe ni app nyingine ambayo itakuwezesha kujifunza lugha na misamiati ya Kiingereza. Ina zaidi ta misamiati 4000 ikihusisha pia tafsiri, mafunzo kwa njia ya video, michezo ya kujifunza. Sambamba na hayo kila siku mwanafunzi atapewa majaribio ya kuzungumza na kuandika ili kupima uwezo wake wa kukumbuka anayojifunza.

App ya Hello English nayo ni mwalimu mzuri wa lugha ya Kiingereza kwa wanaoanza kujifunza. Inajumuisha maeneo yote mtu ambayo anaweza kujifunza kuanzia kwenye misamiati, tafsiri na stadi za kuzungumza, kuandika na kusoma lugha hii kwa ufanisi zaidi.

Punde utakapoipakua na kujisajili utapewa maswali 20 yanayolenga kupima uwezo ulionao katika lugha kabla ya kuanza kupewa mafunzo. Matokeo ya jaribio hilo ndiyo yatakayoonyesha ni hatua gani ya mafunzo mhusika anastahili kuanzia.