Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umejaribu mtindo wa kuchanganya vitenge

Mtindo huu unaweza kutumika katika maeneo na shughuli tofauti tofauti kama vile ofisini, kwenye sherehe na hata kwenye matukio maalum kama vile ya fashion show na nyingine zinazofanana na hizo.PICHA|MAKTABA

Muktasari:

Unachopaswa kuzingatia katika taratibu za uchanganyaji ni kuhakikisha rangi za giza kazi yake ni kupunguza na rangi za muwako ni kuzidisha umbo la mvaaji husika.

Ni msimu wa mitindo ya mavazi yenye rangirangi. Wabunifu wa mitindo wa kimataifa na kitaifa wamekuwa mstari wa mbele katika kuonyesha umahiri wao kupitia mtindo huu.

Ilianza kwenye vipodozi, mavazi na mapambo na sasa ni kwenye vitenge. Je umeshawahi kuvaa mtindo huu? Ikiwa bado wala hujachelewa unaweza kutoka na ubunifu wako na wewe ukaonekana mwenye kuvutia. Na ikiwa huwezi kufanya ubunifu, basi si vibaya ukaonana na wataalamu wa mitindo, kwani wao wana uwezo mkubwa katika kuchanganya rangi.

Katika msimu wa mitindo uliopita tumejionea mtindo wa kuchanganya vitenge ukijumuisha mavazi yenye yaliyobuniwa kwa kutumia vitambaa vyenye rangi za kuwaka. Mavazi hayo yalishamiri sana ambapo takribani wabunifu wa kimataifa na kitaifa waliweza kuonyesha umahiri wao kupita wazo hilo.

Katika msimu huu wa mitindo, wabunifu hasa wa Kiafrika hususani wanaotokea Afrika ya Magharibi walikuja na mtindo mpya wa kuchanganya kitenge na kitenge na kutoa mavazi yenye ladha ya kipekee.

Tofauti ya kawaida mtindo huu hutumia vitenge vyenye rangi za kuwaka na zile zenye rangi za giza hivyo kuleta muonekano wa kuvutia. Kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo , aina hii ya mtindo inaweza kutumika kuongeza ama kupunguza umbo la mvaaji husika.

Katika mahojiano yake na gazeti hili aliyoyafanya hivi karibuni Mbunifu wa mtindo nchini, Ally Remtulah alisema kuwa inawezekana kupangilia rangi katika kitenge na kuboresha umbo la mvaaji husika.

“Ikiwa wewe una umbo la moja kwa moja lakini ungependa kutoka bomba na mtindo huu, unaweza kuchagua kitenge chenye rangi ya giza kwa mfano bluu, kijani au dhambarau halafu kile chenye rangi ya kuwaka kama vile njano pink ama machungwa ukaweka chini. Hii itasaidia kuboresha mwonekano wako,” alisema.

Unachopaswa kuzingatia katika taratibu za uchanganyaji ni kuhakikisha rangi za giza kazi yake ni kupunguza na rangi za muwako ni kuzidisha umbo la mvaaji husika.

Ubunifu huu wa vazi la kitenge umesababisha baadhi ya wapenzi wa fasheni katika nchi za ulaya na Marekani kutumia kitenge katika mavazi yao.

Mke wa raisi wa Marekani Michelle Obama, Mwanamuziki Beyonce Knowles, Mtangazaji maarufu wa kipindi cha mitindo Marekani Giullian Rancic ni baadhi tu ya wadau wa mitindo waliaoamua kuipaisha Afrika kwa kuvaa mtindo wa kuchanganya kitenge.

Mtindo huu unaweza kutumika katika maeneo na shughuli tofauti tofauti kama vile ofisini, kwenye sherehe na hata kwenye matukio maalum kama vile ya fashion show na nyingine zinazofanana na hizo.

Kwa mujibu wa wabunifu mtindo huu upowa wa aina mbili. Kuna ule wa mapande ambapo nguo moja inaweza kushonwa kwa kutumia vitenge vitatu na pia kuna ile ya kuchanga kitenge cha blauzi na kile cha sketi.

Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya

Baruapepe :[email protected]