Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Changamoto za kiafya na kisaikolojia kwa ‘single mothers’

Muktasari:

  • Utafiti ulioandikwa katika mojawapo ya makala za afya ya jamii umeonyesha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa wakinamama wanaolea watoto pasipo waume zao kupata changamoto za kiafya na kisaikolojia, ingawa changamoto hizi zinaweza kutofautiana kutokana na maeneo au mazingira ya maisha wanayoishi. Baadhi ya changamoto hizi ni kama vile magonjwa na matatizo ya afya ya akili ambayo yana uwezekano mkubwa wa kusababisha ugonjwa wa sonona .

Ni kweli kabisa kwamba malezi ya mzazi mmoja wakati wote ni yenye changamoto sana kwa mzazi mwenyewe na hata kwa watoto. Hapa namaanisha malezi ya baba peke yake au malezi ya mama peke yake “single mothers”. Hali hizi hutokea kutokana na sababu tofauti kama vile kufiwa na mwenza, kutengana au kutalikiana kwa wanandoa na kupata mtoto au watoto pasipo kuolewa au kuishi na mwenza.

Utafiti ulioandikwa katika mojawapo ya makala za afya ya jamii umeonyesha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa wakinamama wanaolea watoto pasipo waume zao kupata changamoto za kiafya na kisaikolojia, ingawa changamoto hizi zinaweza kutofautiana kutokana na maeneo au mazingira ya maisha wanayoishi. Baadhi ya changamoto hizi ni kama vile magonjwa na matatizo ya afya ya akili ambayo yana uwezekano mkubwa wa kusababisha ugonjwa wa sonona .

Wanawake waliohusishwa katika utafiti huu walifikia idadi ya 25,000 kutoka nchi tofauti duniani na waliulizwa maswali tofauti yakiwemo yahusuyo hali ya zilivyokuwa ndoa zao, hali za watoto wao na changamoto za malezi wanazo kumbana nazo kila siku, sababu zinazokwamisha utendaji kazi wao wa kila siku, wanazokutana nazo katika maisha binafsi kama vile katika kujipenda, kujijali na kutafuta furaha binafsi. Wanawake hawa waliulizwa pia kutoa maoni kuhusiana na hali za afya zao.

Ingawa utafiti huu ulihusisha kinamama wa nchi tofauti ulimwenguni, asilimia zaidi ya 38 ya kinamama wa nchi za Denmark na Sweden walionyesha kuanza malezi ya mzazi mmoja wakiwa chini ya miaka 50. Asilimia zaidi ya 33 ya wanawake waishio nchini Marekani pia walielezea kuanza kuishi maisha ya malezi ya mzazi mmoja wakiwa chini ya miaka 50. Hali kama hii iliendelea kuonekana kwa akinamama wa nchi za Uingereza kwa asilimia 22.

Kwa ujumla, kumeonekana kuwepo kwa uhusiano mkubwa baina ya malezi ya mzazi mmoja wa kike na kuongezeka kwa matatizo ya kiafya na kisaikolojia katika miaka ya utu uzima na hata maisha ya uzeeni ukilinganisha na kinamama wanaowalea watoto wao wakisaidiana na waume zao. Wanawake walioonyesha kuwa kwenye hatari kubwa ni wale walioanza malezi ya mzazi mmoja mapema zaidi, hususani wakiwa katika umri ya 20 au chini. Wengine ni wale walioendelea kulea watoto peke yao kwa zaidi ya miaka minane na wale wanaolea watoto wawili au zaidi ya wawili wakiwa peke yao, hapa namaanisha pasipo uwepo wa mzazi wa kiume.

Ukubwa wa matatizo haya umeonekana kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa mfano, uhusiano baina ya malezi ya mzazi mmoja na matatizo ya kiafya na kisaikolojia yameonekana kuleta athari hasi chache zaidi kwa wanawake wa nchi za Ulaya tofauti na wanawake wa nchi nyingine.

Hali ilionekana kuwa mbaya zaidi kwa wanawake wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, nchi zinazoendelea au nyingi zilizo masikini, ikiwemo Tanzania. Baadhi ya sababu za kuongezeka au kupungua kwa athari hizi hasi ni kuwepo kwa msaada mkubwa wa ndugu au. Hali hii inaonekana kukosekana kwa familia nyingi za nchi za kimasikini ambapo kila mtu anayemzunguka mama huyu anayelea watoto peke yake ni masikini au asiyejiweza, mwisho wa siku hali ya watoto wake ya elimu, chakula, malazi inazidi kuwa ngumu. Ikumbukwe kwamba hii haimaanishi kuwa wanawake wanaojiweza kimaisha hawaathiriki kabisa, la hasha, wao pia wanaweza kuonyesha athari tofauti hususani za kisaikolojia, na hata watoto wao pia. Hali ngumu ya kifedha, ukosefu wa elimu au elimu ndogo pamoja na ukosefu wa fursa za ajira zilionekana pia kuwa sababu kubwa katika kuongeza athari kwa kinamama hawa.