Prime
ANTY BETTIE: Mke wangu ananipeleka puta faraghani, nifanyeje?

Muktasari:
- Mwanamke huyu mrembo wa sura, tabia na anayejua kumliwaza mwanaume ananipeleka puta tukiwa faragha kiasi kuna wakati ninajisingizia kuumwa.
Anti habari. Awali nilipania niwe na mwanamke hodari tukiwa faragha ambaye atakata kiu yangu kisawasawa. Hivyo siku zote nilikuwa ninamtafuta wa aina hiyo, hatimaye nikampata na sikuchelewa kufunga naye ndoa, ila kinachonikuta usiombe kikukute. Mwanamke huyu mrembo wa sura, tabia na anayejua kumliwaza mwanaume ananipeleka puta tukiwa faragha kiasi kuna wakati ninajisingizia kuumwa.
Wakati tunaanza nililenga kwenye kukonga nyoyo kwa kujamiiana tu na si vinginevyo, hivyo hata kucheza hatukuwa tukitumia muda mwingi, na mwenza wangu amezoea hali hiyo.
Naomba ushauri nifanye nini, maana nahisi kuhemewa.
Hujasema kama mnalingana umri, kwa harakaharaka kama una umri uliosogea kidogo, kisha mwenza wako akawa bado binti hili halikwepeki. Mnatofautiana uwezo kwa namna yoyote ile, wanasema wanaume hawazeeki, lakini niamini mimi, huwezi kutoka na binti mwenye miaka 25 damu changa na miaka yako 55 ukasema mtakwenda sambamba.
Sasa kwa kuwa uhusiano ni zaidi ya kujamiiana na yanahitaji upendo na kuhurumiana, huna haja ya kujisingizia kuumwa tena, mweleze waziwazi kuwa unahitaji huduma hiyo lakini si mashindano mwende taratibu.
Unaweza usimweleze moja kwa moja, lakini jipunguzie dozi kama ilikuwa kwa wiki mara tano, sasa hakikisha inakuwa mara tatu ili utunze nguvu ya ziada utakayoitumia baadaye.
Pia kama ulikuwa unachukua muda mrefu, unaweza kuharakisha kidogo ili usichoke sana kwa sababu ukimaliza pumzi utazidiwa huko mbele ya safari.
Hizi mbinu zote zifanye huku ukitumia maneno mazuri mwenza wako anapong’ang’ania muenende kama zamani.
Mfano unaweza kumwambia: “Una haraka ya nini, tulia nipo kwa ajili yako,”. Ukampa matumaini ili uvute muda ujipange upya, baada ya muda atazoea miondoko hiyo mipya.
Pia ongeza muda wa kucheza, unaweza kuanzisha kutaka kuchuliwa mwili, ilimradi uanzishe vitu vipya vya huba vinavyofanywa na wapendanao wakiwa faragha ili kumpunguza kasi bila kumtoa mchezoni. Ukifanya hivi mara kadhaa atazoea na kuona ni kawaida.
Pamoja na kumueleza hayo bado unapaswa kutafuta mbinu za kuhakikisha unafanya kile ulichokihitaji na mlichokifanya kwa muda mrefu. Hivyo jifunze mbinu mbalimbali za kujamiiana ambazo hazitoathiri mlichokianzisha kwa maana ya mchakamchaka wa faragha.
Mbinu hizo ni pamoja na kujipanga kumridhisha bila kukutana kimwili.
Pia ufanye mazoezi ya ziada kutafuta pumzi, maana uliyonayo imeshazidiwa
Chimba ndani zaidi ujue mwenza wako mambo gani yanamfurahisha zaidi mnapokuwa faragha uwekeze huko, ili kupunguza muda mwingi wa mchakamchaka utakaohitaji kutumika zaidi.
Unaweza kuonana na mtaalamu wa saikolojia kujua nini sababu ya hamu kupungua kiasi cha kukimbizwa ilihali mwanzo ulikuwa unapenda.
Pengine siyo suala la umri mkubwa ni mabadiliko ya kimwili au kiakili kutokana na jambo fulani.
Pia unaweza kuonana na mtaalamu wa hospitali ambaye anaweza kukufanyia vipimo kubaini nini shida.
Kwa kuwa hujasema umri inawezekana una changamoto pengine kuna ugonjwa unaokata hamu hiyo unakunyemelea. Naam! Yapo magonjwa yanayokata kabisa hamu au uwezo wa kujamiiana kwa wanaume.
Pia usifikirie sana kuwa unakimbizwa faragha kwani itaongeza tatizo badala ya kulipunguza. Unaweza kuwa faragha ukianza kuwaza hivyo unapoteza mwelekeo kabisa, hivyo achana na hilo wazo ukiwa kwenye starehe zenu.