Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zijue siku zako za hedhi kuilinda ngozi ya uso

Muktasari:

  • Licha ya kufanya vitu kadha wa kadha kulinda ngozi isiharibike, kuna sababu za kimaumbile, ikiwamo mabadiliko ya homoni ambayo huifanya ngozi kubadilika na wakati mwingine kupata chunusi.

Licha ya kufanya vitu kadha wa kadha kulinda ngozi isiharibike, kuna sababu za kimaumbile, ikiwamo mabadiliko ya homoni ambayo huifanya ngozi kubadilika na wakati mwingine kupata chunusi.

Hili hutokea kwa baadhi ya wanawake kila mwezi wanapokuwa kwenye hedhi. Ili kukabiliana na hali hii, unapaswa kuhakikisha unajua tarehe unazopata hedhi. Ukijua tarehe za kupata hedhi, zikikaribia

kanda uso kwa mvuke.

Yaani chemsha maji yaweke kwenye chombo kipana kama beseni kisha jifunike nguo nyepesi ili kupata mvuke,

hakikisha hayana moto sana ili kuepuka kubabuka. Kama una mashine ya mvuke unaweza kuitumia, mara nyingi zinakuwepo kwenye saluni za kiume.

Ikiwezekana pia osha uso mara mbili kwa siku kwa sabuni unayoitumia, pia usilale na vipodozi na ukiweza punguza kutumia vyenye mafuta.