Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Silaa ‘akomalia’ kusoma makablasha bungeni

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa

Muktasari:

  • Ni mara ya kwanza kwa meya huyo wa zamani wa Manispaa ya Ilala kuingia katika Baraza la Mawaziri ambapo amepewa jukumu la kuongoza Wizara ya Ardhi.

Dodoma. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa leo aliingia bungeni kwa mara ya kwanza akiwa na cheo hicho ambapo muda wote alionekana kusoma makablasha mbalimbali.

Mapema leo Jumatatu Septemba 4, 2023 Silaa aliingia viwanja vya Bunge akiambatana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde na wawili hao walikwenda moja kwa moja kuketi katika maeneo yao mapya.

Hata hivyo, tofauti na Mawaziri na Naibu Mawaziri wengine ambao walikuwa wakipongezana na kupokea pongezi kutoka kwa wabunge ama waliosoma walikuwa wanasoma majibu ya maswali waliyotakiwa kujibu.

Silaa kwa upande alikuwa bize tangu alipoingia na hadi Bunge linaahirishwa bado alikuwa anasoma makablasha na kuandika vitu kwenye makaratasi, hii ni tofauti na mawaziri wengine walioingia kwa mara ya kwanza katika vyeo vipya.

Mapema leo waziri huyo alianzia Mtumba zilipo ofisi za wizara hiyo ambako alikwenda kusaini kitabu kabla ya kurudi bungeni kwenye majukumu mengine.

Leo mchana Silaa na Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa wanatarajia kwenda Mtumba kwa ajili ya kukabidhiwa ofisi zao rasmi huku Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akitajwa kuwa atakabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu katika utaratibu utakaowekwa.