Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi watakiwa kuhamasisha masomo ya sayansi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga

Muktasari:

  • Takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 24 pekee ya wanafunzi wa kike walioko vyuoni wanasoma masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.

Dodoma. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amewataka wazazi na jamii kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi na ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Kipanga ameyasema hayo leo Jumamosi, Februari 11, 2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

“Ubunifu wa wanawake na wasichana ni unahitajika na unachangia kikamilifu katika maendeleo hayo, tunafarijika sana kuona Watanzania hasa wanawake na wasichana wanazalisha bunifu nzuri,”amesema.

Amesema juhudi za Serikali katika kuongeza mchango wa wanawake na wasichana kwa maendeleo ya nchi kupitia sayansi ni pamoja na utoaji wa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, ambayo inatoa kipaumbele kwa wanaojiunga kwenye fani za sayansi.

Ametaja juhudi nyingine ni uanzishwaji wa Mfuko wa Ufadhili wa Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) unaolenga kugharamia wanafunzi wa elimu ya juu wanaojiunga kwenye fani za tiba, uhandisi na hesabu.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 wahitimu 640 wenye ufaulu wa juu kwenye mitihani ya kidato cha sita wamefadhiliwa kusoma programu za sayansi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo ameomba Serikali kuweka nguvu maalum ya kuwaajiri walimu waliosomea masomo ya sayansi ili kuwa na idadi kubwa ya wanasayansi na wabunifu watakaochochea maendeleo ya Taifa.

 “Wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ni wachache, bado tuna changamoto kubwa. Hata katika ripoti yetu ya Kamati ya Bunge (iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii) tulisema kwamba walimu wanaofundisha sayansi ni changamoto ni wachache,”amesema.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Profesa Maulilio Kipanyula amesema siku ya wanawake na wasichana katika sayansi ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015

Amesema kuanzishwa kwa siku hiyo kumetokana na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kufanya utafiti uliobainisha kuwa ushiriki wa wanawake na wasichana katika masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati na ubunifu uko hafifu kutokana na vikwanzo mbalimbali.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 24 pekee ya wanafunzi wa kike walioko vyuoni wanasoma masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.