Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto watatu waliopotea Chalinze wakutwa wamefariki ndani ya gari

Gari ambalo watoto hao wamekutwa wakiwa wamefariki ndani.

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salum Morcase amesema tukio hilo lilitokea baada ya watoto hao kuripotiwa kupotea Julai 9, 2026, na wazazi wao kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Lugoba

Bagamoyo. Watoto watatu waliokuwa wametoweka katika Kijiji cha Lamboni, Kata ya Lugoba, Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani, wamekutwa wamefariki dunia ndani ya gari bovu lililoegeshwa nje ya nyumba, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha vifo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salum Morcase amesema tukio hilo lilitokea baada ya watoto hao kuripotiwa kupotea Julai 9, 2026, na wazazi wao kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Lugoba.

Watoto hao ni Masoud Mwema (9), aliyekuwa na changamoto ya afya ya akili, Mikidadi Halfani (4), wote watoto wa Sophia Chikolo, pamoja na Murath Mbaraka (4), mtoto wa Sauda Hamadi Mustafa. Wote walikuwa wakazi wa Kijiji cha Lamboni, Wilaya ya Chalinze.

Kamanda Morcase amesema baada ya kupokea taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilianza msako wa kuwatafuta watoto hao katika maeneo mbalimbali.

Amesema Julai 10, 2026, majira ya saa 7:30 usiku, Lilahi Mgaza (19), mwanafunzi na mkazi wa Lugoba, alipokuwa akikagua magari mabovu yaliyokuwa yameegeshwa nje ya nyumba yao, aliwakuta watoto hao wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Carina lenye rangi ya fedha (silver), huku milango na madirisha yake yakiwa yamefungwa.

Baada ya kugundua hali hiyo, Lilahi alimjulisha Mohamed Said Mzimba, mmiliki wa nyumba hiyo, ambaye aliwasiliana na Jeshi la Polisi.

Kamanda Morcase amesema miili ya watoto hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Msoga, Wilaya ya Chalinze, kwa ajili ya uchunguzi wa daktari, huku uchunguzi wa kubaini chanzo cha vifo hivyo ukiendelea.

Amewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kufuatilia kwa karibu maeneo wanayochezea watoto ili kuimarisha usalama wao.