Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania sasa kutuma na kupokea Pesa nchi za SADC

Dk Stargomena Tax

Muktasari:

Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom imezindua kampeni ya Vodacom M-Pesa inayoitwa “Dunia Kijiji, Afrika ni M-Pesa” ambayo inawawezesha Watanzania kutuma na kupokea pesa katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom imezindua kampeni ya Vodacom M-Pesa inayoitwa “Dunia Kijiji, Afrika ni M-Pesa” ambayo inawawezesha Watanzania kutuma na kupokea pesa katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
 
Kampeni hiyo ilimezinduliwa jijini Dar es Salaam ambapo ukiacha nchi za Afrika Mashariki imepanua uhamisho wake wa fedha wa Kimataifa (IMT) moaka katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Msumbiji, Swaziland na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  
 
Katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stargomena Tax, ndiye  alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo  ambapo amesema , hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Waziri huyo ambaye aliwahi kuhudumu katika Jumuiya ya SADC, amesema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa huduma hii ni muhimu na waitumie vizuri kujikwamua kiuchumi katika ukanda huo wa SADC.
“Nikiwa SADC tulianzisha mfumo wa sekta ya fedha jumuishi kwa nchi hizo, hivyo kilichofanywa na M-Pesa ni sehemu ya ule mpango. wamenigusa moyo wangu.
“Mbali na ukuaji wa kiuchumi, lakini hatua hii imesaidia mtu mmoja mmoja kwani inarahisisha gharama za kutuma pesa na urahisi kwani hii pesa zinamfikia mlengwa kwa wakati huo huo ambao anadhamiria kutuma,” alisema Waziri Tax.
 
Waziri Tax pia aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambaye ndiyo mdhibiti wa pesa za kimataifa kwa kufanya kazi na waendeshaji wa simu ili kuhakikisha kuwa malipo na malipo ya kimataifa yanakuwa salama.
 
“Naipongeza BoT kwa kutoa leseni kwa Vodacom chini ya kifungu cha16 (3) ya kanuni ya ubadilishaji wa nje ya 2022 ambayo inaruhusu Watanzania na M-Pesa kutuma pesa zaidi ya Afrika Mashariki na sasa kwa nchi za SADC,” alisema Waziri Tax.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania, Epimack Mbeteni alisema M-Pesa baada ya kufanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki sasa wameamua kuongeza wigo huo kwa nchi za SADC.
 
Mbeteni amesema safari ya Vodacom M-Pesa IMT ilianza mnamo 2014 kwa kuungana na Kenya, mnamo 2019 kufanikiwa kutuma na kupokea pesa kote Afrika Mashariki na kupokea pesa kutoka nchi zaidi ya 200 duniani.