Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataalamu waliotambua Murburg wailetea ‘dili’ Tanzania

Muktasari:

  • Kituo cha mafunzo ya ulinzi na usalama wa vimelea kwa wataalamu wa maabara Afrika Mashariki chazinduliwa Tanzania. Kituo hiki kitatoa mafunzo kwa wataalamu kutoka Kenya, Uganda na Tanzania.

Dar es Salaam. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za Afrika zenye vituo vya kikanda vya mafunzo ya umahiri kwa watalamu wa maabara katika ulinzi na usalama wa vimelea.

Kituo hicho kilichopo chini ya Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kimezinduliwa leo Jumatatu Aprili 3, 2023 na kitakuwa kikitoa mafunzo kwa watalaamu wa maabara wa Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema uwepo wa kituo hicho nchini umezidi kudhihirisha uwezo wa Tanzania katika kutambua magonjwa ikiwemo Murburg.

Amesema baada ya Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Africa (CDC) kutaka kuanzishwa kwa kituo hicho katika ukanda wa Afrika Mashariki nchi zote ziliomba, lakini Tanzania ikaonekana kuwa na uwezo zaidi ya kupata hadhi hiyo.

Amesema, “Kituo hiki kimekuja wakati mwafaka maana tayari tumeshaonyesha mfano kwenye kutambua kwa haraka ugonjwa kama ambavyo ilitokea Kagera tukaweza kujua ni ugonjwa gani na tuudhibiti vipi.

“Magonjwa sasa hayana mipaka hivyo katika kupambana nayo nchi wanachama wa WHO zinapaswa kujenga uwezo wa kuzuia tusipate magonjwa pili tuweze kujindaa, hatua ya tatu ni kutambua ugonjwa.

Ummy amesema kwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kuwatumia wataalamu wa ndani kutambua ugonjwa hivyo mafunzo hayo ya kimataifa ya ulinzi na usalama wa vimelea yataongeza ufanisi katika eneo la maabara na jinsi ya kushughulikia sampuli.

“Tumeona kule Kagera miongoni mwa waliokufa ni mtaalamu wa maabara, ilitokana na kushindwa kujikinga sasa tunapopata mafunzo ya aina hii ni wazi yataenda kuwaimarisha watu wetu wa maabara sio tu kuchunguza sampuli bali hata uangalifu dhidi ya vimelea,” amesema Ummy.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Zablon Yoti ameipongeza Tanzania kwa hatua hiyo na kuahidi kuwa shirika hilo litatoa kila aina ya ushirikiano utakaohitajika kuhakikisha kituo hicho kinafanya kazi iliyokusudiwa kwa ufanisi.