Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Washikiliwa kwa tuhuma za kutaka kusafirisha kobe 201

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege, ASP Martin Otieno akiwaonyesha waandishi,  mojawapo ya kobe zaidi ya 200 waliokamatwa juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  (JNIA) ambao wanadaiwa kuwa walikuwa wakisafirishwa kupelekwa  nchini Malaysia. Katikati ni SP Amedeus Tesha na PC Monica Likoko. Picha na Venance Nestory

Muktasari:

Alisema ufungaji huo ulifanyika ili kwenye mashine ya ukaguzi isijulikane kilichomo ndani ya mabegi hayo.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kutaka kusafirisha kobe hai 201 wenye thamani ya Sh30.4 milioni waliokuwa kwenye soksi kwenda Kaula Lumpa, Malaysia.

Kamanda wa Polisi JNIA, Martin Otieno aliwataja waliokamatwa kuwa ni mkazi wa Kariakoo, David Muungi (36) na mkazi wa Kidongo Chekundu Zanzibar, Mohamed Suleiman Mohamed (43).

Otieno alisema kobe hao aina ya Indian Star, waliwekwa watatu hadi sita ndani ya soksi na kisha kwenye pampasi kubwa ndani ya mabegi matano.

Alisema ufungaji huo ulifanyika ili kwenye mashine ya ukaguzi isijulikane kilichomo ndani ya mabegi hayo.

Kamanda Otieno alisema mizigo hiyo ilipofika katika eneo la uchambuzi juzi saa 4.30 usiku, kikosi kazi kiliyatilia shaka mabegi hayo yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda chini Malaysia kupitia Dubai kuwa huenda yakawa na nyara za Serikali.

Otieno alisema juhudi zilifanyika ili kuwatambua wamiliki wa mabegi hayo na walikamatwa na baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi cha Uwanja huo kwa ajili ya upekuzi.

“Watuhumiwa hawa walikamatwa katika eneo la ukaguzi wa mwisho wa abiria na kupelekwa kwenye eneo la uchambuzi wa mizigo na waliyatambua mabegi yao,” alisema Otieno.

Watuhumiwa hao walipohojiwa na polisi walidai kobe hao waliwatoa Visiwa vya Comoro na Ushelisheli lakini polisi wanahisi hawakutoka huko, bali mwambao wa Pwani.

“Tulipoendelea kuwahoji walidai wanampelekea mteja wao anayeishi Kaula Lumpa ambaye jina lake hatuwezi kulitaja  kutokana na upelelezi unaoendelea,” alisema Otieno.

Februari 27, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, polisi walikamata kobe wadogo 250 wakitaka kusafirishwa kwa njia ya magendo kwenda Malaysia.

Juni 24, kwenye Uwanja wa JNIA polisi pia walimkamata raia wa Kuwait, Hussein Mansoor akiwa na kobe 173 aliokuwa akiwasafirisha kuelekea nchini kwake.