Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanyamapori waingia mitaani Longido kusaka maji

Tanki la maji ambalo limepasuliwa na tembo kijiji cha Karao Longido.

Muktasari:

  • Wilaya ya Longido kwa miaka mitatu mfululizo imekosa mvua za kutosha hali iliyosababisha ukame na upungufu wa chakula na maji.

Longido. Ukame uliochangiwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi, umeanza kusababisha wanyamapori kuingilia mitaani, kusaka maji kwa kung'oa mabomba ya na kuvunja matanki ya maji Wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Wanyama hao ambao ni pamoja na tembo, wameng'oa bomba kubwa la maji Kijiji cha Olbomba na kuvunja tanki la maji shule ya msingi Resimita, huku wengine wakivunja matanki makubwa ya mawili Kijiji cha Karawa.

Akizungumzia uvamizi huo, Ofisa Mifugo na Mabadiliko ya tabia nchi wilaya ya Longido, Nestory Daqqaro amethibitisha leo Oktoba 18, 2022 amesema ni kwa sababu ya ukame wa muda mrefu.

Daqqaro amesema katika Kijiji cha Kitumbeini wanyama wadogo wakiwepo pofu wameingia katika makazi wakisaka maji na kusababisha Wananchi kuwapa.

"Tuna changamoto kubwa kwani mwaka wa tatu mvua zimenyesha chini ya kiwango, mito yote imekauka lakini pia hata Malisho yamepotea kutoka na Ukame," amesema.

Amesema hadi sasa zaidi ya mifugo 38,720 imekufa wakiwepo twiga wanne, pundamilia 18 na swala wawili waliozama kisimani wakisaka maji.

Mkurugenzi wa shirika la Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Zakaria Faustine ameshauri kufanyika jitihada za kuokoa wanyamapori na mifugo.

Amesema tayari kuna mradi wa kukusanya taarifa hali ya mabadiliko ya tabia nchi na Mazingira, utunzwaji mazingira na vyanzo vya maji kwa maarifa ya asili ili kukabiliana na hali hiyo.

"Shirika la Umoja wa Mataifa UNDP kupitia program ya miradi midogo inayofadhiliwa na mfuko wa Mazingira duniani (GEF) wanasaidia asasi ya MAIPAC na mashirika madogo 12 tunadhani tutapata suluhu ya changamoto hizi," amesema.

Mmoja wa wanakijiji, Neema Mollel ameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili jamii yao ya kifugaji na wanyamapori wasiathirike zaidi ikiwepo pia kusaidia kuondoa majani vamizi katika ardhi yao.