Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi 193 wawekwa karantini kufuatiliwa viashiria vya Marburg Kagera

Aliyekaa katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Tumaini Nagu akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Kagera juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali ili kuzuia ugonjwa wa Marburg usiendelee kusambaa kwa wananchi.

Muktasari:

  • Wagonjwa watatu wa Marburg hali yao inaendelea vizuri na hukuna wagonjwa walioongezeka na 193 wako karantini.

Bukoba. Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Tumaini Nagu amesema wagonjwa watatu wa Marburg wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika na hakuna maambukizi ya watu wengine huku akisema kuwa watu 193  wamewekwa karantini.

Dk Nagu ameyasema hayo leo Machi 23, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba juu ya mikakati ya Serikali ya kupambana na ugonjwa huo.

"Wagonjwa watatu wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri na mmoja alikuwa na hali mbaya lakini kwa siku ya leo Machi 23 hali yake inaendelea kuimarika.

Ametaja mikakati ya Serikali ya kupambana na ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha wananchi juu ya kupambana na ugonjwa huo kwa kunawa mikono na maji safi tiririka yenye sabuni.

Pia kutogusana mikono na kutoa taarifa kwa viongozi waliopo kwenye maeneo yao wanapobaini mtu mwenye dalili za kutapika au kutapika damu, kuharisha au kuharisha damu, kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili kuumwa kichwa na joto la mwili kupanda.

Aidha mkakati mwingine ni pamoja na kuweka vifaa vya kupima joto la mwili, vitakasa mikono na maji tiririka yenye sabuni maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vituo vya magari, maeneo ya soko kwenye viwanja vya ndege na bandarini na sehemu za biashara.

Aidha amesema watu wapatao 193 waliokuwa wamechangamana na watu waliobainika kuwa na ugonjwa wa Marburg mkoani hapa kati yao 89  wakiwa ni watumishi wa afya  wamewekwa karantini.

 Dk Nagu amesema kuwa, baada ya watu wanane Halmashauri ya Bukoba Vijijini kuugua ugonjwa wa Marburg na watano kupoteza maisha kuanzia Machi 16, mwaka huu walianza kufuatilia wale wote waliochangamana nao na mpaka sasa watu 193 wamewekwa karantini.

“Watu wapatao 193 ambao walichangamana na wagonjwa wa Marburg wamewekwa karantini na kati yao 89 ni watumishi wetu wa afya na tangu tumeanza kuwafuatilia hakuna mwenye dalili ya ugonjwa huu na tunaendelea kuwaangalia kwa karibu ndani ya siku 21,” amesema Dk Nagu.

Kwa upande wake  Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini amesema kama kiongozi wa dini anahamasisha  mambo matatu, juu ya ugonjwa wa Marburg,  ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya nao kuutoa kwa waumini na  kuwaambia waumini wao wasipaniki.

Naye Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi Kaskazini Magharibi,  Abednego Keshomshahara amesema kuwa, wamewashauri waumini wao kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia kwa wataalamu wa afya ni pamoja na kuelimsha waumini kufuata tahadhari zinazotolewa na wataalamu hao.