Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi 18,000 kunufaika na mradi wa maji Biharamulo

Muktasari:

  •  Zaidi ya wananchi 18,000 watanufaika na mradi wa maji wa Biharamulo baada ya kukamilika kwake. Serikali imefanya uwekezaji wa Sh325 milioni kwa ajili ya kukamilisha mradi huo wa Biharamulo.

Biharamulo. Takribani wananchi 18,031 katika vijiji vinne vya kata ya Kabirizi iliyopo wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera watanufaika na mradi wa maji utakaogharimu Sh325 milioni hadi kukamilika kwake.
Meneja wa wakala wa maji vijijini na usafi wa mazingira (Ruwasa) wilaya ya Biharamlo, Lucas Matina amesema kuwa mradi huo ulianza kujengwa Julai mosi, 2020 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2021 na wananchi hao watanufaika.
Amevitaja vijijini vitakavyonufaika kuwa ni pamoja na Kabindi, Nyamugogo, Chebitembe na Kikomakoma na kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mitatu ambayo itagharimu Sh3 bilioni.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Merryprisca Mahundi amesema katika bajeti ya mwaka 2021/22, serikali imetenga Sh47 bilioni kwa ajili ya miradi ya maji na fedha hizo zinasaidia kukamilisha miradi iliyoanza kujengwa.
“Kuna wakandarasi ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miradi zaidi ya mmoja na kushindwa kukamilisha kwa wakati. Hakuna mkandarasi ataongezwa muda wa kumaliza mradi wa maji, wajitahidi kumaliza kwa wakati,” amesema Mahundi.
Mahundi amesema lengo la Wizara ya Maji ni kumtua mama ndoo kichwani na kuona muda waliokuwa wanatumia kuchota maji wanafanya shughuli za uzalishaji na wanafunzi waliokuwa wanatumia muda wao kwenda kuchota maji wanajisomea.
Kwa upande wake, mkazi wa kijiji cha Kabindi, Dafroza Charles amesema kukamilika kwa mradi huo kutawapunguzia adha ya kusafiri zaidi ya kilomita tatu kwenda kufuata maji.
Naibu waziri Mahundi yuko kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera ambapo anatembelea miradi mbalimbali ya maji mkoani humo.