Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi watumia kivuko cha mawe

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Sawe iliyopo Wilaya ya Hai wakivushwa baada ya daraja lililokuwepo mto Marire kusombwa na maji.

Muktasari:

Wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari Sawe ,iliyopo katika kijiji cha Kyeer ,Kata ya Machame Magharibi ,Wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro wanalazimika kutumia kivuko cha mawe ili kuvuka mto Marire baada ya daraja lilokuwepo kusombwa na maji mwaka jana.

Hai. Wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari Sawe ,iliyopo katika kijiji cha Kyeer ,Kata ya Machame Magharibi ,Wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro wanalazimika kutumia kivuko cha mawe ili kuvuka mto Marire baada ya daraja lilokuwepo kusombwa na maji mwaka jana.

 Mbali na kuwekwa kivuko hicho cha mawe wanafunzi hao hulazimika kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema wanaopita kuwavusha huku wengine wakilazimika kutoka na wazazi wao majumbani ili waweze kuwavusha katika mto huo ambao huwa na maji mengi hasa kipindi cha mvua.

Wakizungumza na Mwananchi,wazazi wa wanafunzi hao wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwawekea kivuko ili kuwanusuru watoto wao na hatari ya kusombwa na maji pindi wanapovuka wenyewe.

Rehema Munuo ,Mkazi wa kijiji hicho amesema kukosekana kwa daraja hilo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwao huku wakihofia watoto wao kusombwa na maji hasa katika kipindi hiki.

"Tunaomba serikali itusaidie kutengeneza daraja maana tunapata shida kila siku kuwavusha watoto wetu kwenda shule asubuhi na jioni na wakati mwingine wakivuka wenyewe tunaogopa wasisombwe na maji maana huu mto unabeba maji mengi yanayotoka milimani,"

Edward Mushi ambaye pia ni mwananchi wa kijiji hicho ameiomba serikali kuangalia utaratibu wa kuwawekea angalau kivuko ili kunusuru maisha ya watoto wao katika kipindi hiki ambacho mvua zinatarajia kunyesha.

 "Tunaomba serikali itusaidie maana ni mwaka mzima sasa tumekuwa tukipata hizi shida baada ya daraja letu kusombwa na mafuriko mwaka jana , tunaiomba serikali itusaidie  kuweka daraja katika huu mto,"

Naye diwani wa kata hiyo,Martin Munis amesema tangu  mwaka jana mafuriko yalivyobeba madaraja katika wilaya ya Hai,hali  ni mbaya kwani  wanafunzi wanashindwa kuvuka kwenda shuleni mpaka wazazi wawavushe asubuhi na jioni.

"Kutokana na hali hii ombi langu kwa serikali tunaomba ituwekee kivuko   ili shughuli za kijamii zisisimame hasa wakati huu ambao mvua ni nyingi huku mlimani kwasababu watu wanashindwa kwenda mashambani na wakati mwingine wagonjwa wanashindwa kufika hospitali,"