Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi kidato cha kwanza wasakwa nyumba kwa nyumba Geita

Muktasari:

  • Msako wa nyumba kwa nyumba wakuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti katika Shule ya Sekondari Izumacheli umezaa matunda baada ya wanafunzi kuongezeka kutoka wanne walioripoti wiki iliyopita hadi kufikia wanafunzi 40 leo Jumatatu 16, 2023.

Geita. Msako wa nyumba kwa nyumba pamoja na matangazo yaliyofanywa mtaani yakuwataka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Izumacheli waripoti shule imesaidia idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi wanne walioripoti wiki iliyopita hadi kufikia wanafunzi 40 leo Jumatatu Januari 16, 2023.

Shule hiyo iliyoko maeneo ya kisiwani ilipangiwa wanafunzi 88 kuanza kidato cha kwanza mwaka huu lakini mwamko kuripoti ulikuwa mdogo hali iliyomlazimu Katibu Tawala Wilaya ya Geita, Thomas Dime kuagiza watendaji wa vijiji na kata pamoja na afisa elimu kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria shuleni.

Akizungumza na mwananchi kwa njia ya simu mkuu wa shule hiyo, Edward Nkwabi amesema jitihada zilizofanywa na viongozi zimezaa matunda ambapo wanafunzi wa kidato cha pili wameongezeka kutoka 26 hadi kufikia 33.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Izumacheli, Faustine Samike amesema msako bado unaendelea ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wanaanza masomo.

Shule ya Izumacheli ilianza mwaka 2022 na ipo kwenye moja ya kisiwa katika Ziwa Victoria ikitegemea wanafunzi kutoka visiwa vingine vya Butwa na Lulegeya ambapo awali kabla ya kujengwa wanafunzi walilazimika kusafiri hadi kata jirani ya Nkome iliyoko nje ya Ziwa.
Ili wanafunzi waweze kuhudhuria shuleni wanalazimika kupanga vyumba ‘geto’ mtaani kutokana na shule hiyo kuwa kisiwani na boti inayopita maeneo hayo hufika majira ya saa sita mchana hivyo kuwa changamoto kwa wanafunzi wanaotoka kwenye visiwa vingine vya Lulegeya na Butwa.