Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamwangukia DPP kumaliza kesi meno ya tembo

Muktasari:

  • Washitakiwa watatu wamemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili waingie kwenye makubaliano ya kumaliza kesi inayowakabili ya kusafirisha vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh4.6 bilioni.

Dar es Salaam. Upande wa mashitaka katika kesi ya kusafirisha vipande 660 vya meno ya tembo yenye thamani ya Sh4.6 bilioni inayowakabili washtakiwa 13 umesema washtakiwa watatu kati yao wamemwandikia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kumwomba wamalize shauri linalowakabili.

Washtakiwa walioingia makubaliano hayo na DPP ni Ally Sharif, Abasi Hassan na Kassim Hassan.

Wakili Mkuu wa Serikali, Felix Kwetukia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 30, kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini wamepokea barua kutoka kwa washtakiwa hao wanataka kuingia makubaliano na DPP ili waweze kumaliza shauri hilo.

Ndipo wakili wa Utetezi, Jamuhuri Jonson aliiomba mahakama hiyo ianze kuhesabu siku 30 kuanzia leo ili washtakiwa hao waweze kufanya majadiliano hayo na DPP waweze kumaliza shtaka hilo.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga amesema washitakiwa hao wameandika barua kwa ajili ya majadiliano waweze kumaliza kesi hiyo hivyo amearisha shauri hilo hadi Machi Mosi, 2023 shauri hilo litakuja kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia majadiliano hayo yamefikia wapi na Machi Mosi, 2023 imepangwa kusikilizwa ushahidi.

Mbali na washtakiwa hao watatu wengine ni Victor Mawalla, Haruna Kassa, Solomon Makuru, Musa Ligagabile, Khaflan Kahengele, Ismail Kassa, Peter Nyanchiwa, John Buhanza na Mussa Mussa wote no wakazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na nyara za serikali bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori, ambazo ni meno hayo yenye thamani ya zaidi ya Sh4.6 bilioni

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa na mtandao wa uhalifu wa ujangili ambao unajihisisha na kuuza na kununua, kupokea na kuhamisha, kusafirisha nyara za serikaki ambazo ni meno ya tembo.