Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamiliki mabasi waeleza walivyojipanga kushindana na SGR

Muktasari:

  • Wamiliki wa Mabasi wamesema licha ya treni ya umeme kuanza safari zake katika baadhi ya mikoa, wataboresha huduma zao kuhakikisha wanashindana na usafiri huo.

Dar es Salaam. Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (Taboa) kimesema kuanza kwa safari za treni ya umeme hakutaathiri biashara yao, kwani wanaamini abiria wasiopenda mwendokasi bado wapo.

Juzi Juni 14, 2024 safari ya kwanza ya treni ya abiri ya umeme ilianza kutoka Dar es Salaam hadi  Morogoro kwa nauli ya Sh13,000 kwa daraja la kawaida ambayo ni sawa na nauli ya mabasi.

Pia Julai 25, 2024 treni hiyo itakwenda hadi Dodoma kwa nauli ya Sh31,000 kwa daraja la kawaida.

Kutoka kwenye stesheni ya SGR Dar es Salaam hadi ila ya Kihonda, Morogoro treni hiyo ilitumia saa 1:54 ambapo ilianza safari saa 12:01 asubuhi na kuwasili saa 1:55 !asubuhi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), safari za treni hiyo zitakuwa kila siku, lakini iwe mara ngapi kwa siku itategemea na mahitaji ya abiria.

Hata hivyo kwa kuanzia, siku ya kwanza kulikuwa na safari nne, mbili za Dar es Salaam na mbili za Morogoro, hali iliyoibua sintofahamu kuhusu biashara ya mabasi na kuwepo na taarifa kwamba imeanza kutetereka.

Leo Juni 16, 2024 akizungumza na Mwananchi Digital, Ofisa Habari wa Taboa, Mustapha Mwalongo amesema hawajaathirika chochote tangu kuanza kwa usafiri huo Ijumaa iliyopita.

"Mpaka sasa hakuna athari yoyote kwenye mabasi, hata hivyo tunafahamu kutakuwa na ushindani wa kibiashara, hivyo tunachokifanya ni kuboresha huduma zetu ili kushindana na treni ya umeme.

"Taboa tumekuwa tukiwahamasisha watoa huduma wetu kuendelea kuboresha huduma ili kuingia kwenye ushindani," amesema.

Kuhusu muda wa treni wa saa 1:54 kuwapa 'mzuka' abiria wengi kutumia usafiri huo na kuachana na mabasi ambayo hutumia saa 4 na 4:30 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mwalongo amesema hilo sio tatizo kwani wapo abiria wasiopenda mwendokasi.