Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wajumbe CCM watakiwa kuachana na chuki, majungu

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulamu

Muktasari:

  • Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulamu amewataka wanachama wa CCM kufanya kazi kwa ushirikiano na kuachana na chuki, hila na majungu ili waendelee kukijenge chama hicho.

Shinyanga. Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulamu amewataka wanachama wa CCM kufanya kazi kwa ushirikiano na kuachana na chuki, hila na majungu ili waendelee kukijenge chama hicho.

Gulamu ameyasema hayo leo Oktoba Mosi, 2022 wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa wilaya uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa ambapo amewataka wanachama wote kuacha majungu na chuki ili waendelee kukijenga chama.


Amesema licha ya kwamba amestaafu, ataendelea kuwa mtiifu na viongozi wakimuhitaji wasisite kumuhusisha kwenye jambo lolote, atatoa ushirikiano bado anakipenda chama chake hicho.


“Mimi nitaendelea kuwa mtiifu siku zote kwa sababu nakipenda chama changu, hivyo nawaomba wanaCCM tupendane kwa dhati, tufanye kazi kwa ushirikiano tuondoe chuki, hila na majungu. Nawaomba sana, chama hiki kinahitaji upendo, hakihitaji unafiki,” amesema Gulamu.


Gulamu amesema anastaafu akiwa hajagombana na mwanachama yoyote na anakipenda chama na wanachama wote. Amesema amelelewa CCM, hivyo anaheshimu uamuzi wowote na ameupokea kwa mikono miwili.


“Tunatakiwa tuwe watulivu ndani ya CCM mimi ni binadamu tunategemeana ukiondoa uongozi kutoka kwangu isije ikawa nikishiriki misiba ionekane ni shida,nikiongea na mwanachama kosa, ndugu zangu mimi nitaendelea kuwa mwanachama uhusiano wangu na watu nitaulinda kwa gharama yeyote mimi sina dhambi na chama changu CCM tusisuguane tujitahidi kuondoa dosari zetu,” alisema Gulamu.


Mwenyekiti huyo mstaafu amewataka wajumbe kuchagua viongozi watakaofanya nao kazi kwa maslahi ya chama, pia ambao watakipeleka chama mbele ili kiweze kuendelea kushika dola.