Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wajasiriamali wataka sikukuu na wiki yao ya maonyesho

Mjasiliamali Neema Mtei (mwenye fulana nyeupe) akiwa kwenye kibanda chake katika maonyesho ya wajasiriamali yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini hapa. Picha na Sute Kamwelwe.

Muktasari:

  • Wajasiriamali wameomba Serikali iwepo siku yao ya maonyesho ya bidhaa zao kama ilivyo nanenane na sabasaba huku wakitaka kuwa na maonyesho ya walau wiki nzima.

Dar es Salaam. Wajasiriamali waliokutanishwa kwenye maonyesho ya bidhaa zao yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam wameomba kutengewa siku yao maalumu kama ilivyo sikukuu za sabasaba na wakulima nanenane.

Wakizungumza na mwananchi kwa nyakati tofauti baadhi yao wamezungumzia changamoto ya ukopaji kupitia vikundi jambo ambalo wanadai ni changamoto.

Wameyabainisha hayo leo Septemba 12, 2023 ikiwa ni siku ya pili ya maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya CRDB benki Foundation kupitia programu ya imbeju kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ilala.

Neema Mtei mkulima na mzalishajI wa Uyoga kutoka jijini hapa anasema mbali ya kutaka siku ya maonyesho ya kitaifa, ameziomba taasisi zinazotoa mikopo ziangalie suala la utoaji kwa watu binafsi na si vikundi kama ilivyo.

"Tunaomba tuwe tuna uwezo wa kupata mikopo mtu mmojammoja. Suala la vikundi mimi hapana hadi leo sijawahi. Kuna wengine wagumu kulipa hivyo tunataka tusimame sisi kama sisi," amesema Neema alipokuwa akifanya mahojiano na Mwananchi.

Mariam Nachecha, ambaye ni mzalishaji wa pilipili pamoja na achali ya dagaa pia ametamani ukopaji binafsi kwakuwa inamfanya kuwa huru zaidi nakuondoa usumbufu. Mbali na hilo pia ameiomba Serikali kuwatafutia masoko nje ya nchi kwakua wanazalisha bidhaa adimu.

Pia, ameliomba Shirika la Viwango TBS, kuwaandalia sehemu za usindikaji mbali na makazi ya watu jambo ambalo kwa mtu mmoja ni ngumu kwakuwa hawana mitaji.

Vilevile mjasiriamali Rashid Mdee amesema, "Tunatamani ziwepo siku zetu za maonyesho nchi nzima kama ilivyo sikukuu ya maonyesho ya wakulima nanenane na biashara sabasaba ili tutanue wigo wetu wa kibiashara."

Mdee ambaye ni mzalishaji wa sabuni za kufulia na kusafishia vyombo amesema maonyesho hayo ni fursa ila yaongezwe siku ziwe nyingi zaidi.

"Tunatamani iwepo wiki ya mjasiriamali kwa sababu tunapata wateja na tunajitangaza vilevile tunapata fursa ya kusajiliwa," amesema Mdee.

Haijaishia hapo, Erasmus Ukulele muuzaji wa mafuta ya kupikia ya Soya amesema maonyesho hayo yamewapatia soko na uwanda mpana wa kuelimishana kama wafanyabiashara wadogo.

"Tunahitaji mafunzo zaidi ya Brella, TRA na TBS kwetu sisi na napendekeza maonyesho yaende hadi mikoani pamoja na kutengewa siku yetu," amesema Ukulele.