Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara soko dogo Kariakoo wagoma kupisha ujenzi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Wakati mkandarasi wa kukarabati soko kuu la Kariakoo akipatikana, baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo wamegoma kupisha ukarabati huo.

Dar es Salaam.Wakati mkandarasi wa kujenga soko dogo la Kariakoo na kukarabati lile kubwa lililoungua na moo akiwa amekabidhiwa mkataba wa kuanza kazi rasmi, wafanyabiashara katika soko dogo wametoa masimamo wao wa kutoondoka sokoni hapo.

 Makabidhiano ya kuanza ujenzi kati ya mkandarasi ambaye ni Estim, yalifanyika leo Desemba 24 sokoni hapo kati ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam, Hassan Rugwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Estim, Bashir Jushmy.

Mwananchi iliyokuwa eneo hilo, ilishuhudia makabidhiano hayo,huku yakishuhudiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri na watendaji wengine kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakala wa barabara Vijijini na Mjini (Tarura).

Hata hivyo katika makabidhiano hayo hakukuwepo na uwakilishi wowote kutoka upande wa wafanyabiashara,sio wa soko lililoungua wala soko hili dogo.

Wakati wafanyabiashara hao wakiweka msimamo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija, amesema ni lazma wahame na watawahamishia soko la Kisutu na lile la Machinga Complex.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Hussein Magaeli amesema wameshangaa kuona mkandarasi akikabidhiwa kuanza kazi wakati kikao cha cha juzi kati yao na Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla walikubaliana kuwa wafanye mazugumzo kwanza na Mkuu wa Wilaya kuhusia na utekelezaji wa mradi huo utakavyokuwa bila kuathiri biashara zao.

"Mazungumzo yetu kati ya mkuu wa Wilaya yalikuwa pamoja na mambo mengi tujue nmna gani tutaondoka hapa na vipi tutarudi,hivyo kwa hatua hiyo ni wazi kwamba tumepuuzwa na serikali ya mkoa kuamua kufanya inavyoona," amesema Magaeli.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa uhamaji katika eneo hilo unatakiwa uwe wa kimaandishi na sio kwa kusema tu kwa mdomo ambapo baadaye wataweza kukosa ushahidi na eneo lao kupewa watu wegine.

Kwa upande wake mfanyabiashara Angeline Agustino, amesema kuondolewa bila utaratibu sokoni hapo ni kutaka kuwarudisha wanawake kwenye shughuli zisizo halali.

"Hapa sokoni kumesititiri wanaake wengi wakiwemo wajane na qale qaliokuwa wanafanya shughuli zisizo halili zikiwemo za kuuza miili,sasa leo kuambiwa tunatakiwa tuondoke, pasipokujua tunaelekea wapi ni kuwarudisha wanawake kulekule," amesema Angelina.

Mwishehe Dizeru, ambaye ni msemaji wafanyabiashara hao, amesema katika utekelezaji wa mradi huo wanaona wanaendelea kutengwa kwani mbali na kilichofanyika jana cha mkandarasi kukabidhiwa kazi bila wao kuwepo.

Akijibu hoja hizo, DC Ludigija amesema mazungumzo na wafanyabiashara hao anatarajia kuyafanya Jumatatu na kuingoza kuwa suala la kuandikishiana pia liko kwenye mchakato, kwa kuwa lengo la mradi huo ni kuona wafanyabiashara wengi wanachukuliwa kuliko ilivyo sasa.

Hata hivyo, kiongozi huyu alibainisha kuwa wana taarifa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapi wanapinga kuhama hapo na kuwahamasisha wengine kutokana na kuwa na vizimba zaidi ya kimoja ambapi wanawakodishia wengine, hivyo wanajua wazi wakaondolewa na kurudishwa watavikosa vizba hivyo.