Wadau afya ya uzazi wataka uwepo sheria ya mimba zitokanazo na kubakwa
Muktasari:
- Wametoa kauli hiyo katika j katika mkutano wa kuadhimisha siku ya huduma ya utoaji mimba salama,ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba 28.
Wadau wa masuala ya afya ya uzazi wametaka uwepo wa sheria nchini ya kuruhusu utoaji mimba zitokanazo na vitendo vya kubakwa.
Wametoa kauli hiyo katika Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kuadhimisha siku ya huduma ya utoaji mimba salama, ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba 28 ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Kutoa mimba kwa njia salama ni huduma inayookoa maisha’
Wakati wanaharakati wakija na hoja hiyo Sheria ya Tanzania Kanuni ya Adhabu Penal Code) Sura ya 16. inakataza k utoaji wa mimba kwa njia yoyote ile, isipokuwa katika hali zinazohitaji utaratibu wa kitabibu, kama vile kuokoa maisha ya mama anayebeba mimba.
au pale mimba imekuwa chanzo cha maradhi ambayo hayawezi kutibika vinginevyo na yanaweza kuathiri afya ya mama.
Sheria hii hukataza pia ushiriki wa mtu yeyote katika kutoa mimba, ikiwa ni pamoja na yule anayetaka kutoa mimba, mtoa mimba,na mtu yeyote anayeshiriki au kuunga mkono.
Aidha adhabu ya kosa la kutoa endapo mtuhumiwa akikukutwa na hatia anaweza hukumiwa hukumu hadi ya kifungo cha maisha
Hoja za wadau
Wadau hao wamehoji kama aliyebaka anafungwa miaka 30 jela kwa makosa ya ubakaji , kwanini mimba iliyotokana na kubakwa iwe halali na kutaka wanaotunga sheria wafikirie ni namna gani hali hiyo inavyomuthirika muhusika hadi mtoto anayekuja kuzaliwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi wa Shirika linalojidhughulisha na masuala ya afya ya uzazi(WGRN), Nondo Raymond ambao ndio walikuwa wenyeji wa mkutano huo,amesema wakati wakija na hoja hiiyo jamii inapaswa kujua kuwa zipo sababu mbalimbali za watu kutoa mimba kwa njia isiyo salama ikiwemo hiyo ya kubakwa.
Nondo amezitaja kati ya hizo zipo za kubakwa, kubeba mimba ambayo muhusika hakuwa ametarajia na kwa sababu nchi hairuhusu utoaji mimba wamekuwa wakienda kupata huduma hiyo vichochoroni na mwisho wa siku kupoteza maisha au kuharibu kizazi hali inayowaathiri hadi baadaye kutokuja kushika ujauzito tena.
“Kutokana na sababu kama hizi, tunaona kuna haja ya kuwepo sheria itakayoruhusu waathirika wa haya kupata huduma kama ilivyo huduma nyingine zinazohusiana afya ya uzazi.
Kwa mujibu wa Nondo, nchi ambazo zimeridhia sheria hii, ukiangalia hata takwimu zao zitakanazo na vifo vya uzazi zipo chini, hivyo kama Tanzania inavyopambana kutokomeza vifo hivyo ni vema ikaridhia sheria hiyo ambayo ipo pia katika sheria za kimatifa ikiwemo ile ya ‘Maputo Protacal’
Naye Mwanasaikolojia,Sylivia Sostenes, amesema madhara ya watu kuzaa watoto ambao walitokana na mimba zisizotarajiwa ni pamoja na kuwachukia,kutowalea ipasavyo na hivyonkuchangia ongezeko la watoto mitaani,baadhi kuachika kwenye ndoa zao kwa sababu tu alibakwa na wengine kupata matatizo ya afya ya akili.
AnitaDoto Samson, akiwakilisha vijana amesema wanafurahi tayari kuna mwongozo wa huduma ya afya kwa vijana, lakini ni vema huduma pia ya mtu ambaye anataka kutoa mimba asiyoihitaji nayo iwe kwa wazi badala ya kusubiri hadi awe ameshaiharibu huko mtaani na kufika hospitali hoi ndio ahudumiwe.
Monica Patrick kutoka Shirika la Women and Youth Movement(Woyomo), la mkoani Simiyu amesema kwa kuwa bado jamii haijaelewa madhara makubwa yaliyopo katika vitendo vya utoaji mimba zisizo salama, kuna haja ya kuendela kuibuliwa kwa visa mkasa ili ione madhara na madhila wanayopita wahusika labda wanaweza kuelewa kwa nini wanaharakati wanapigania haki hiyo kuwa sheria.
Vilevile ametaka mashirika yanayopambania haki hizo kuwatengeneza kisaikolojia waathirika ili iwe rahisi kwao kufunguka kwa kuwa ni vitendo ambavyo mtu akivifanya jamii inamuona mkosaji na mkosefu wa maadili.