Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waandishi, majirani waaga mwili ‘house girl’ aliyeuawa Dar

Muktasari:

  • Majirani wakishirikiana na waandishi wa habari wamefanikisha kuandaliwa kwa mwili wa msichana wa kazi za ndani Aneth Kassim (17) anayedaiwa kuuawa na mwajiri wake Tabata Kimanga Februari 8, 2023.

Dar es Salaam. Waandishi wa habari wameshirikiana na majirani katika maandalizi na taratibu za kuaga mwili wa aliyekuwa msichana wa kazi za ndani Aneth Kassim (17) na kisha mwili wake kusafirishwa leo kuelekea Ngara kwa maziko.

 Kaka wa binti huyo, Imani Benjamin ndiye ndugu pekee aliyefuata mwili akitokea kijiji cha Mkikomelo wilayani Ngara hali iliyowafanya waandishi wa habari kushirikiana na majirani waliojitokeza.

Mwili wa Aneth umesafirishwa leo Februari 18 mchana kwa gari kuelekea Ngara na unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu kijijini kwao Mkokomelo.

Aneth ambaye alizaliwa mwaka 2005, alifikwa na umauti Februari 8 akiwa na mwajiri wake Diana Joseph anayetuhumiwa kumuua Anneth majira ya saa mbili usiku nyumbani kwake na kumfikisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidai alimkuta binti huyo amejinyonga bafuni.

Akizungumza kwa niaba ya Clouds Media waliofanikisha kusafirisha mwili huo, Gea Habib amesema walifanya harambee ikiwa ni mchakato wa kuweza kufanikisha mazishi ya binti hiyo.

“Tunashkuru Watanzania wametufanikisha hili na kutuchangia Sh3.34 milioni fedha ambazo tumelipa gharama za mwili kukaa mochwari kwa wiki moja, dawa, vibali, mwili kuandaliwa na tukanunua sanduku, nguo za Aneth.

“Kuna kiasi kimebaki namkabidhi Imani kwa ajili ya kusaidia nyumbani na kila kitu kimeshamalizwa hapa Sh1.204 milioni,” amesema Gea.

Akitoa shukrani Imani amesema, “Nawashkuru Watanzania kwa msaada wao na Clouds Media kwa kuwa nami bega kwa bega namshkuru pia Afande Simba aliyenisaidia kusafiri kutoka ngara mpaka hapa kuja kutambua mwili wa mdogo wangu, mliotoa Mungu awaongezee.”