Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vilio, simanzi vyatawala maziko ya bibi harusi mtarajiwa

Muktasari:

  • Bibi harusi huyo, Rehema Chao (39) amezikwa yeye na mama yake mzazi, Agness Chao (75) kijijini kwao Nganyeni, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro huku vilio na simanzi vikitawala katika maziko hayo ambayo yamefanyika siku ya harusi yake leo, Desemba 2, 2023 na  kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji.

Moshi. Hatimaye bibi harusi mtarajiwa aliyefariki ajalini, akitokea kwenye sherehe yake ya ‘sendoff,’ Rehema Chao (39) amezikwa leo, Desemba 2, 2023 kijijini kwao Nganyeni, Kata ya Mwika, Kaskazini, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Rehema amezikwa yeye na mama yake mzazi, Agness Chao (75) kijijini hapo, huku vilio na simanzi vikitawala katika maziko hayo ambayo yamehudhuriwa na mamia ya waombolezaji.

Novemba 28, mwaka huu bibi harusi huyo mtarajiwa, akiwa na mama yake mzazi na ndugu wengine pamoja na mfanyakazi wa nyumbani, Irene Shija (15), wakiwa wanatokea kwenye sherehe  ya kuagwa  mkoani Morogoro walipata ajali eneo kichwa cha Ng'ombe, wilayani Mwanga.

Ajali hiyo inadaiwa kutokea baada ya Rehema ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari hilo, kukwepa shimo na hivyo kugongana na lori.

Rehema alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua, mkoani Morogoro, sherehe ya kumuga ilifanyika Novemba 24, 2023; na mara baada ya sherehe hiyo, walianza safari ya kuja nyumbani kwao Marangu, Moshi.

Rehema aliambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ambayo ingefanyika, leo Desemba 2 mkoani Arusha.

Akihubiri katika ibada hiyo ya maziko, Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Calvin Koola ameitaka familia hiyo kumtazama Mungu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao.

Koola amesema huu si wakati wa watu kufikiria kwa nini wamekufa bali ni kipindi cha familia na waombolezaji wengine kumtazama Mungu na kutambua kuwa ni mipango ya Mungu.

"Katika maisha tunapaswa kuishi kama vile tunakufa leo, na niiombe familia, msiba huu usiwaondoe kwa Mungu, endeleeni kumtegemea na kumtazama yeye, maana yeye (Mungu) ndiye anayejua sababu za haya," ameasa Mchungaji huyo.

Ameongeza kuwa: "Aman Mollel mtazame Mungu na mwambie yeye ajua, na msimnung'unikie Mungu kwa haya, mshukuruni kwa yote kwani ameamua kuchukua harusi ya pili na kachanganya na ya tatu akasema zifanyike leo na ikaishia hapo."

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sua, Mwazani Jambaraga amesema msiba huo ni zaidi ya maumivu kwa kuwa alikuwa hodari, mchapakazi na kwamba Sua imepoteza jembe, hata hivyo hawana namna zaidi ya kukubali mpango wa Mungu.

Given Chao ambaye ni pacha wa Rehema, amesema marehemu alisema Shule ya Msingi Marieni, Shule ya Sekondari Vunjo na baadaye Shule ya Sekondari Arusha, kisha kusomea ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambako alitunukiwa shaha ya taaluma hiyo.