Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Vilio vyatawala mazishi ya bibi harusi, wenzake

Muktasari:

Miili ya wana ndugu wanne waliofariki katika ajali ya gari juzi Jumatano akiwamo bibi harusi mtarajiwa, inazikwa leo nyumbani kwao Chimala, wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya


Mbarali. Vilio na simanzi vimetawala nyumbani kwa familia ya Jackson Mwandunga wilayani  hapa Mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili miili minne ya familia hiyo akiwamo aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa, Diana Mwandunga.

Miili hiyo imewasili leo Ijumaa asubuhi Juni 21, 2019 ikitokea Hospitali ya Rufaa Mbeya ilikokuwa imehifadhiwa baada ya  watu hao  kufariki dunia kwenye ajali ya gari ndogo juzi Jumatano eneo la Machimbo barabara kuu ya Mbeya-Makambako.

Wengine waliofariki dunia  kwenye ajali hiyo ni Faraja Mwandunga, James Mwandunga na mtoto wa Faraja, Jacton (2) wakati waliojeruhiwa ni Ibrahimu Mwandunga na Nico Mwandunga.

Ajali hiyo ilitokea baada ya ndugu wa  familia hiyo, kumuaga ‘Send off’ Diana katika sherehe iliyofanyika Jumamosi iliyopita ya Juni 16 nyumbani kwao Chimala, Mbarali na Juni 26, 2019 ilitarajiwa kufanyika Send Off nyingine jijini Dar es Salaam kisha ndoa Juni 29, 2019.

Vilio vimetawala baada ya majeneza yaliyobeba miili ya ndugu hao ilipowasili nyumbani kwa ajili ya maziko yatakayofanyika leo Ijumaa.

Miongoni mwa wahudhuriaji wa mazishi hayo ni bwana harusi Elisante  Edward ambaye mara zote anaonekana kutokwa machozi huku akisaidiwa na ndugu kumfariji.

Kutoka idadi kubwa ya waombolezaji waliojitokeza, shughuli ya kuaga miili hiyo imehamishiwa  uwanja wa mpira wa stendi mpya Chimala.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea