Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vikwazo upatikanaji elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu

Muktasari:

  • Mwanafunzi mmoja kati ya wanne wenye ulemavu alifanikiwa kujiunga kidato cha kwanza 2022, wakati wengine wakishindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali.


Dar es Salaam. Mwanafunzi mmoja kati ya wanne wenye ulemavu alifanikiwa kujiunga kidato cha kwanza 2022, wakati wengine wakishindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali.

Ripoti ya Takwimu za Elimu Msingi (BEST 2021) inayotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilionyesha wanafunzi wenye ulemavu 4,951 walimaliza darasa la saba mwaka huo, lakini asilimia 23 walifanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Msingi wa takwimu hizo unachagizwa na taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa kwenye mkutano na walemavu, akisema wanafunzi 1,157 walemavu wamejiunga kidato cha kwanza mwaka huu, huku akiwataka wadau kuhakikisha wanawezesha kundi linaloanza elimu ya msingi lisiendelee kuporomoka hadi ngazi ya vyuo.

Ripoti ya BEST inaonyesha kwa mwaka 2021, wanafunzi wa kidato cha kwanza 3,040 ni matokeo ya wanafunzi 55,758 waliomaliza darasa la saba 2020, sawa na asilimia 94 ya waliokwama kuingia sekondari.

Wanafunzi hao ni wale wanaosoma shule binafsi na umma nchini kote kutoka makundi ya watu wenye ulemavu wa kuona, kusikia, kuona na kusikia, wenye ulemavu wa ngozi, ulemavu wa viungo, ulemavu wa akili, ulemavu wa akili na viungo, wenye usonji, uoni hafifu na usikivu mgumu (hard hearing).

Stella Jairos (57) mwenye ulemavu wa macho na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (Swauta) anasema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari iandae mkakati wa kuendesha vipindi maalumu katika runinga, redio vinavyohusu watu wenye ulemavu waliofanikiwa.

“Lengo itakuwa ni kujenga ushawishi. Unajua wakiona au kusikia mtu mwenye ulemavu amefanikiwa, wazazi wengi wataanza kuwatoa watoto wao ndani wakijua kumbe watakuwa hazina yao baadaye, wako wengi wamefanikiwa sana,” anasema Stella.

Stella, aliyepata Stashahada ya Ualimu mwaka 1994/96 katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Duce), anaeleza changamoto yake ya kuona ilimlazimu kupata msaada wa kusomewa na rafiki zake wakiwa kidato cha kwanza hadi cha nne Shule ya Sekondari Korogwe “Dhana potofu iliyopo ni kwamba kusomesha mtoto mwenye ulemavu ni kupoteza nguvu na mali tu, namshukuru Mungu wazazi wangu (Mzee Jairosi na Vumilia) ambao hawakuwa na elimu, walikabiliana na vikwazo vyote katika elimu na makuzi yangu,” alisema Stella.

Rose Tesha, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Watu wenye Ulemavu (ADD) anasema sababu nyingine ni pamoja na hali ya umaskini wa familia kugharimia elimu, umbali wa shule, ukosefu wa programu za lishe shuleni na jamii, walimu kutotambua umuhimu wa elimu hiyo.

Mwananchi imefanya mahojiano na familia ya Ama Hassani Kiswagala (73), mtaa wa Lindi, makutano ya barabara ya Shauri Moyo, Ilala jijini Dar es Salaam anayeishi na Wastara Said (40) na mwanawe Zuhura Salehe (23), wote wenye ulemavu wa usonji kwa miaka zaidi ya 20 na hawajapata fursa ya kwenda shule.

“Wastara kabla ya kumzaa huyo Zuhura alisoma Uhuru Mchanganyiko, lakini akakwama darasa la nne, sijui ilikuwaje, wazazi wake wote walipofariki ndio nikaanza kukaa naye hadi akamzaa Zuhura, sasa nikiwaacha pamoja huwa wanagombana, tukipata tunakula, tukikosa tunalala,” alisema Ama.

Hata hivyo, Wastara anayezungumza kwa tabu alisema yuko tayari kurudi shule, sawa na Zuhura, mwanawe anayeonekana mchangamfu wakati wote. Baadhi walisema wakati mwingine Wastara amekuwa akiomba msaada wa pesa kwa wasamaria wema ili kujikimu mahitaji yake, ikiwamo urembo wa kusuka, huku baadhi ya majirani wakisema kutokana na hali walizonazo wamekuwa wakienda kuomba msaada wa chakula katika soko la Kariakoo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Repoa, Dk Donald Mmari alisema kundi la wenye ulemavu linapokosa elimu hukosa fursa ya ushiriki katika mkondo wa shughuli za maendeleo.

Agizo na utekelezaji

Katika hotuba yake wiki iliyopita, Rais Samia alisikitishwa na kitendo cha wanafunzi hao kuishia njiani, licha ya juhudi za Serikali kuwaunganisha ngazi ya awali hadi chuo kikuu.

“Sasa utaona walioanza kuandikishwa elimu ya awali ni wengi kuliko wanaoingia kidato cha kwanza, jinsi tunavyotoa elimu tunataka hawa tuliowaandikisha twende nao hadi wafikie masomo ya elimu ya juu.”

Rais Samia alisema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa ajili ya wenye ulemavu, mwaka 2021/22 ikiwezesha ujenzi wa mabweni 50 katika halmashauri 50, huku ikitarajia kujenga mabweni zaidi, kufufua vyuo vya ufundi stadi na ununuzi wa vifaa visaidizi.

Mkuu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Mwalimu Shezeria Kiwango alisema Serikali imeamua kuwekeza katika elimu ya wanafunzi hao ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Kwa sasa vifaa si changamoto, tunaishukuru serikali, mwikitio wa wanafunzi ndio bado, sisi tunaendelea kuwasajili wakati wowote, kwa mwaka huu kuanzia Januari hadi Machi tumeshapokea watoto nane darasa la kwanza na watano shule ya awali.Tunashauri wajitokeze.”

Rasheed Maftah, Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu alisema katika kutekeleza agizo la Rais, tayari idara hiyo imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema na Afua (unafuu) Stahiki kwa watoto wenye ulemavu.

“Katika mwongozo huu tumeshazindua, utasaidia kutambua mapema kila mtoto mwenye ulemavu nchini kote kuanzia umri wa mwaka mmoja, akifikia umri wa kuanza elimu ya awali tunazungumza na mzazi au mlezi wake, ili aweze kumwandikisha shuleni, kwa hiyo kazi hiyo tumeshaanza,” alisema Maftah.

Ndoto na sheria

“Machi 7, mwaka huu, Rais Samia alitembelea Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa na kukutana na mwanafunzi wa kidato cha sita mwenye ulemavu wa viungo na kuzungumza, Emmanuel Mzena aliyemuahidi kutimiza ndoto zake za kuanzisha taasisi ya kuhamasisha wazazi kupeleka mtoto mlemavu shuleni.