Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za ubaharia

Arusha. Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimewataka vijana mbalimbali kuweza kuchangamkia fursa katika kupata utaalamu bora katika programu za mafuta, gesi, makapteni wa meli na uchukuzi.

Hayo yamesemwa leo Septemba 13 jijini Arusha na Makamu Mkuu wa  chuo hicho   Utawala , Fedha  na Mipango Dk Lucas Mwisila wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano  la pili la kitaifa la wiki ya ufuatiliaji na tathmini.

Amesema chuo hicho kinazalisha wataalamu  wenye uwezo wa kufanya ufuatiliaji, tathmini na tafiti sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kuleta matokeo chanya kazini.

Ameongeza chuo hicho kimekuwa kikitoa mitaala mbalimbali na kufanya utafiti kwa ajili ya uboreshaji ili kuongeza tija katika kozi mbalimbali na kuweza kuwaandaa vijana waliobora na waliobobea katika fani hizo ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi na umakini mkubwa.

“Lengo la kutoa kozi zenye wataalamu wa aina hii ni ili kuwezesha jamii kupata huduma zenye tija kwao na Taifa, kwani unapofanya kitu bila kufanya ufuatiliaji na tathimini huwezi kujua kama ni kizuri au la  na unapofahamu kasoro zake zinarekebishwa mapema na kutoa huduma zinazokidhi vigezo vinavyohitajika katika jamii,” amesema Dk Mwisila

Ameongeza moja ya faida za wataalamu kuzingatia ufuatiliaji na kufanya tathmini, husaidia mazao yanayopatikana ndani ya bahari, kama mwani, mafuta, umeme au samaki yote yafike katika masoko kwa wakati.

"Wataalamu ambao tumekuwa tukitoa chuoni hapa wana ubora wa kutoa huduma ndani na nje ya nchi na tunajivunia  hill kwani kimekuwa ni chuo cha kuigwa kutokana na namna ambavyo tumeboresha utendaji  kazi wetu," amesema

Naye Mmoja wa wataalamu wa masuala ya ufuatiliaji na tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulamavu, James Mallya amewataka vijana wanaohitimu masomo yao kwenye vyuo  mbalimbali  kupewa mbinu za kuachana na utegemezi wa ajira za serikali, badala yake wajiunge na kozi ya ubaharia na uhandisi zenye wataalamu wachache duniani, ili kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuajiriwa kiurahisi.

Amesema kwa Tanzania vijana hawana sababu ya kukosa mafunzo hayo, sababu tayari kuna Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ambacho kinatoa kozi hizo na kusaidia vijana wengi wanaohitimu kuajiriwa kwenye vyombo vya majini ndani na nje ya nchi, sababu ya uchache wa wataalamu hao.

“Ifike mahali  vijana wetu waache kuona masomo ya kupangiwa na wazazi wao au ndugu, bali waangalie soko la ajira, hizi kozi wataalamu wa  ubaharia ni wachache na wataalamu zaidi wanahitajika ili kuziba pengo lililopo, ukisoma lazima utapata ajira au utajiajiri mwenyewe kwenye bahari zetu na maziwa na kuondokana na kulalamikia serikali juu ya ajira,” amesema.