Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana waishio mazingira hatarishi kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali

Muktasari:

Mradi wa miaka mitatu wa “Youth Can” unatekelezwa katika mikoa mitano ya Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Arusha na Unguja visiwani Zanzibar na takribani vijana 600 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kupatiwa mafunzo.

Dar es Salaam. Taasisi ya SOS Children’s Village imezindua mradi wa kuwawezesha vijana walio katika mazingira hatarishi kupata ujuzi wa ujasiriamali na mafunzo ya uanagenzi ili waweze kujitegemea wenyewe katika mahitaji ya msingi.


Mradi huo wa miaka mitatu unatekelezwa katika mikoa mitano ya Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Arusha na Unguja visiwani Zanzibar na takribani vijana 600 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kupatiwa mafunzo.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanyika leo Desemba 21, 2022 jijini SDar es Salaam, mkuu wa miradi ya SOS Children’s Village, Anthony Binamungu amesema mradi huo umewajumuisha vijana waliolelewa na SOS pamoja na wale wanaoishi mazingira hatarishi.


Amesema mradi huo unaojulikana kama “Youth Can” (vijana wanaweza), unatekelezwa na taasisi hiyo katika nchi 48 barani Afrika na tangu ulipozinduliwa mwaka 2017, umewafikia vijana 14,000 na kubadilisha maisha yao.


“Mradi huu tunauzindua pia hapa Tanzania na tunatarajia kwamba utawanufaisha vijana wengi. Tunashirikiana na wadau mbalimbali ambao wanatupatia fursa kwa ajili ya vijana wetu kwenda kujifunza kwa vitendo katika kampuni zao,” amesema Binamungu.


Amesema katika miaka 30 ya kuanzishwa kwa shirika hilo, wamefanikiwa kuwalea vijana wengi ambao wamefanikiwa kuwa vijana na katika malezi hayo wamegundua kwamba vijana hao wanahitaji stadi za kimaisha na kitaaluma zitakazowawezesha kuleta maendeleo katika jamii.


“Kwa kutambua hilo, tumekuja na mkakati mahsusi wa kuwajengea uwezo pamoja na kuwatafutia fursa za kupata ajira nchini nan je ya nchi,” amesema Binamungu na kuongeza kwamba wanawaunganisha wadau mbalimbali katika kuhakikisha vijana wanapata ajira.


Kwa upande wake, mratibu wa maendeleo ya vijana taifa wa SOS Childrens Village, Samson Anthony amesema shirika hilo limeingia makubaliano na kampuni ya DHL ambayo inawapokea vijana kwa ajili ya kuwapatia mafunzo kwa vitendo ili kuwapa uzoefu.


“Youth Can imelenga kwenda mbele saidi kufanya kazi na wadau wengine zaidi ya DHL. Kwa hiyo tunashirikisha wadau wengi Zaidi ambao tutafanya nao kazi katika maeneo matatu ya huu mradi ambayo ni mentorship (ulezi), mafunzo na kufanya kwa vitendo,” amesema.


Mmoja wa vijana wanaonufaika na mradi huo, Glory Kitomari amesema amefanya mafunzo ya uanagenzi katika kampuni ya DHL kwa mwaka mmoja, hivyo amepata uzoefu na maarifa ambayo yatamsaidia kupata kazi sehemu nyingine.


“Sasa hivi najua ujuzi nilioupata utanisaidia kupata kazi sehemu nyingine kwa sababu nimeshajua mazingira ya kazi na itakuwa rahisi kwangu, ninajua jinsi ya kufanya kazi na namna ya kujiweka nikiwa kazini,” amesema Kitomari ambaye amelelewa na SOS huko Zanzibar.