VIDEO: Adakwa kwa kukeketa wanafunzi wawili

Muktasari:
- Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa kijiji cha Chiwondo wilayani Chamwino, Chidalo Tagoo (64) kwa tuhuma za kuwakeketa wanafunzi wawili wa darasa la tatu wenye umri wa miaka 12 na 13.
Dodoma. Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa kijiji cha Chiwondo wilayani Chamwino, Chidalo Tagoo (64) kwa tuhuma za kuwakeketa wanafunzi wawili wa darasa la tatu wenye umri wa miaka 12 na 13.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martine Otieno amesema tukio hilo lilifanyika Julai 12,2022 lakini liliripotiwa polisi Julai 20.
“Tunamshikilia mama mmoja mtu mzima wa kijiji cha Chiwondo Chidalo Tagoo (64) kuwafanyia ukatili watoto wawili wa kike mmoja ana miaka 13 na mwingine ana miaka 12 wote wanasoma darasa la tatu, hawa ni watoto wamefanyiwa ukeketaji bila ridhaa yao,”amesema.
Amesema wanaendelea na upelelezi na wakiukamilisha watamfikisha mtuhumiwa mahakamani huku akitoa wito kwa Watanzania kuepuka ukeketaji kwa kuwa una madhara kwa watoto hao wa kike.