Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utafiti wabaini ongezeko la watoto mitaani

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga

Muktasari:

  • Umaskini na ukatili majumbani ni sababu kuu mbili zinazoongeza idadi ya watoto mitaani.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua ripoti ya utafiti inayoonyesha idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani inaongezeka.

Utafiti huo uliohusisha mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Mwanza na Arusha umebaini idadi ya watoto 6,393 nyakati za mchana na 1,385 usiku.

Akizindua utafiti huo uliosimamiwa na Shirika linalopambana na watoto wa mitaani la Railway-RCA, leo Mei 14, 2018 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga amesema kuna kila sababu ya kutafakari sababu zinazofanya watoto mtaani kuongezeka.

"Watoto wa mtaani sio wa Serikali wala mashirika ya kiraia peke yake, Watanzania wote tutafakari jambo hili kwa sababu hakuna mtaa uliowahi kuzaa mtoto," amesema.

Amesema umaskini na ukatili majumbani ni sababu kuu mbili zinazoongeza idadi ya watoto mtaani.

Akiwasilisha utafiti huo uliofanywa chini ya Mradi wa Kizazi kipya, Mtafiti kutoka RCA, Fredrick Mbise amesema utafiti huo pia umebaini vijana 4,202 wa miaka kati ya 18 -19 wanaishi na kufanya kazi mitaani.