Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unesco kufanya utafiti matumizi ya intaneti nchini


Muktasari:

  • Unesco kuwezesha utafiti unaoangalia matumizi ya intaneti nchini. Utafiti huo utafanyika katika kipindi cha miezi mitatu na ripoti yake kutumika katika uandaaji wa sera mbalimbali

Dar es Salaam. Tume ya Tehama Tanzania imeingia makubaliano na Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Elimu na Sayansi na Teknolojia (UNESCO) imepanga kufanya utafiti kuhusu matumizi ya intaneti nchini na namna huduma hiyo inavyoweza kuwafikia watu wengi katika kufiki lengo la kuwa taifa lenye uchumi wa kidijitali.

Utafiti huo utafanywa ndani ya miezi mitatu na unalenga kuangalia upatikanaji wa huduma ya intaneti na matumizi yake kwenye jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Dk Nkundwe Mwasaga amesema utafiti huo utakuwa wa kwanza kufanyika nchini ambapo pamoja na taarifa hizo kuhitajika Unesco zitasaidia pia katika uandaaji wa sera hasa katika kipindi hiki ambacho huduma nyingi zinafanyika kwa tehama.

Amesema kulingana na Unesco intanenti ni huduma ambayo kila mtu anapaswa kuipata lakini hali iko tofauti kwa Tanzania ambapo bado kuna idadi ndogo ya waliofikiwa na huduma hiyo.

“Unesco wenzetu wana viashiria ambavyo ndivyo tutavitumia kwenye utafiti huu. Hatuangalii uwepo wa intaneti pekee bali imesambaa kwa ukubwa kiasi gani, je ni jumuishi  makundi yote kwenye jamii yanatumia au kwa wengine ni tatizo.

 “Tutakachokibaini kwenye utafiti tutatumia kwenye uandaaji wa sera mbalimbali pamoja na kuwapa jumuiya za kimataifa ili waone wanatuongezea nguvu katika eneo gani. Kama nchi tunapaswa kufahamu kuwa sasa hivi intaneti ni huduma muhimu,”alisema Dk Mwasaga.

 Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa Unesco Tanzania Michel Toto amesema ushirikiano huo wa shirika hilo na Tanzania ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya katika makao makuu ya shirika hilo Februari mwaka jana.

 “Bahati nzuri mimi ndiye niliyeupokea ugeni ule miongoni mwa mambo aliyoomba Unesco kuisaidia Tanzania katika eneo la teknolojia, leo niko hapa kusaini makubaliano na Tume ya Tehama kuanza kulifanyia kazi eneo hili.

 “Tunakwenda kushirikiana kufanya utafiti huu imani yetu ni kwamba matokeo yake yatakuwa msaada katika nyanya tofauti kwanza kupata takwimu za watumiaji wa intaneti, eneo lililofikiwa na taarifa hizi zitatumika katika uandaaji wa sera na miongozo mbalimbali,” amesema Toto.