Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA yazindua kituo kipya cha kodi Kariakoo

Muktasari:

Kituo hicho kitakuwa na majukumu saba ikiwemo, kutoa elimu kwa mlipakodi, kusajili biashara mpya, kutoa Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) namba, kufanya makadirio ya kodi, ukaguzi wa kodi za ndani na kufanya malipo.

Dar es Salaam. Katika kusogeza huduma kwa wateja, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imezindua kituo kipya cha kutoa huduma kwa mlipakodi cha Shaurimoyo jijini hapa kikiwa ni cha kwanza kwa mkoa wa kikodi Kariakoo.

Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 14, 2022 mgeni rasmi wa hafla hiyo, Naibu Kamshna wa TRA,  Mcha Hassan Mcha  amesema mkoa wa kikodi wa Kariakoo ni wa kimkakati ulioanzishwa Julai mwaka 2018 hivyo kituo hicho kinalenga kuongeza ufanisi wa makusanyo ya kodi.

‘’Tulifanya hivi kwa lengo la kusogeza huduma kwa eneo la Kariakoo ambalo ni kitovu cha biashara nchini na mataifa jirani na mkoa huu unatoa kodi katika eneo la ukubwa wa kilomita 3.47 ikiwa na mipaka ya barabara ya Lumumba, Morogoro, Jangwani Kawawa na Pugu na sekta kuu ni biashara,” amesema.

Amesema katika mkoa huo wenye jumla ya wafanyabiashara 30,000 unakuwa kwa kasi ikilinganishwa na baadhi ya mikoa mingine na kwamba kuanzishwa kituo hicho ni muendelezo wa serikali kuboresha mazingira ya biashara kwa mkoa huo.

Mgeni rasmi huyo amesema mkoa wa kikodi wa kariakoo kwa mwaka wa fedha uliopita 2020/2021 ulishika nafasi ya sita kwa kuingiza mapato kitaifa kati ya mikoa 31 ya idara ya kodi za ndani wakichangia Sh148 bilioni sawa na asilimia 3.5 ya makusanyo yote ya ndani ya sh4.2 trilioni.


“Kwa mwaka huu 2022/23 kwa Kariakoo wamejiwekea lengo la kukusanya Sh174 bilioni na katika robo ya mwanzo ya mwezi julai hadi Septemba wamefanikiwa kukusanya Sh 39.1bilioni sawa na asilimia 99.9,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Massawe ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuwasogezea huduma huku akieleza mafanikio waliyopata TRA, yanatokana kutekeleza wajibu huo bila kutumia nguvu.

“Naomba dhana hiyo iendelee na kwakuwa sisi kazi zetu kila siku tunafunga na kufungua biashara hivyo tunomba elimu kwa mlipakodi irudi kwa nguvu zaidi nab ado tunahitaji vituo kama hivi geographia ya Kariakoo ni kubwa,” amesema.