Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chande amng’ata sikio bosi TRA

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad  Chande amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Alphayo Kidata kuweka mikakati madhubuti ya kuwasimamia watumishi  wa taasisi hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na uadilifu.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad  Chande amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Alphayo Kidata kuweka mikakati madhubuti ya kuwasimamia watumishi  wa taasisi hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na uadilifu.


Naibu waziri huyo ametoa maelekezo huyo baada ya Serikali kubaini kuna baadhi ya watumishi hawazingatii taratibu na sheria zilizowekwa na badala yake wamegeuka miungu watu kwa kujenga uhasama dhidi ya walipakodi wakati wa kutekeleza wajibu wa kukusanya kodi.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumapili Novemba 13,2022, kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya matembezi ya mbio za shukrani kwa mlipakodi, tukio lilifanyika viwanja vya  Gymkhana amesema pamoja na kufikia malengo wanayojiwekea watumishi wa tasisi hiyo ni lazima wachungwe kama hawazingatii taratibu.


“Kamshina Mkuu wa TRA, fanyeni kazi kwa weledi na uadilifu na kushirikiana kwa hali na mali, na kiudugu na walipa kodi na Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya Tehama kuona inakuwa rahisi kwa walipa kodi na wakusanyaji kupunguza changamoto,” amesema Chande

Chande amesema watumishi wa aina hiyo nilazima wachukuliwe hatua za kinidhamu huku akimuelekeza kamshina wa taasisi hiyo kufanya usimamizi madhubuti kwa watumishi wake.


Aidha, amewahimiza Watanzaia kuendeleza utamaduni na wajibu wa kulipa kodi kwa hiayari kwa maendeleo ya Taifa.


Naye Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata licha ya kukiri kuyafanyia kazi maagizo hayo lakini alielezea wiki ya mlipa kodi inalenga kuwashukuru Watanzania katika kusukuma guruduma la maendeleo ya nchi.


 “Kwa mwaka 2021/2022, Serikali ilitupa lengo la kukusanya Sh22.45 trilioni na tumefanikiwa kwa asilimia 99.1 baada ya kukusanya Sh22.28 trilioni ambayo ni niongezeko la Sh4 trilioni kutoka makusanyo ya mwaka 2020/2021 tuliyokusanya Sh 18 trilioni na tumeona ni wajibu kurudi kwa walipakodi wetu kuwaambia asante,” amesema Kidata


Kidata amesema pamoja na mafanikio hayo taasisi hiyo imejiwekea malengo kwa mwaka 2022/2023 kukusanya Sh24 trilioni huku akieleza matunda yameanza kupatikana kwa kota ya kwanza ya mwaka wameanza kufikia mafanikio baada ya kukusanya asilimia 105 ya lengo.


“Tumekusanya Sh5 trilioni kwa hiyo tunaendelea kuwashukuru na tumejipanga kwa mwaka huu wa fedha tufanye vizuri zaidi na walipakodi ambao ni chachu muhimu katika maendeleo ya Taifa,” amesema Kidata