Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TPSF yawanoa wadau kukabiliana na ujangili

Meneja Mradi wa Tuhifadhi Maliasi kutoka TPSF, Godfrey Mondi akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau kutoka sekta ya benki na mawasiliano juu ya kukabiliana na biashara haramu ya Wanyamapori. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Msaada la Marekani (Usaid) chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili.



Dar es Salaam. Katika kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori nchini, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imewakutanisha wadau wa sekta ya benki na mawasiliano kuwajengea uwezo wa kukabiliana na ujangili nchini.

 Lengo la mafunzo hayo ni kuwapa mbinu za kutambua viashiria vinavyoashiria uhamishwaji wa fedha zinazofanyia biashara haramu ya wanyamapori pamoja na mawasiliano ambayo yanaweza kusaidia kuwakamata majangili.

Hayo yamesemwa leo Desemba 9, 2023 na Meneja Mradi wa Tuhifadhi Maliasili kutoka TPSF, Godfrey Mondi, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa benki na sekta ya mawasilinao nchini, kuhusiana na kukabiliana na ujangili.

Mondi amesema mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la Msaada la Marekani (USAID) chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili, unaotekelezwa na TPSF, yamelenga kutoa uelewa kwa wafanyakazi kuhusu utakatishaji fedha kwa njia ya mialama unaofanywa na majangili kupitia biashara ya wanyamapori.

"Mafunzo hayo yatawaongezea uwezo wa kupambana na kuzuia biashara haramu ya maliasili lakini pia kuongeza uelewa wa namna gani majangili na wafanyabiashara hao wanaweza kusafirisha mizigo haramu kutoka eneo moja kwe eneo linguine," amesema Mondi.

Amesema wanatambua Tanzania inategemea sekta ya utalii katika kuchangia pato la Taifa ndio maana wameamua kutoa mafunzo hayo kwa taasisi hizo za fedha na mawasilinao ili wasaidiane kukabiliana na biashara hiyo haramu ya usafirishaji wa wanyamapori.

"Usafirishaji haramu wa wanyamapori ni biashara ya nne kwa ukubwa, ikiongozwa na biashara ya usafirishaji wa binadamu, dawa za kulevya na masuala ya utakatishaji wa fedha.

“Ndio maana tumewapa mafunzo wadau wa benki na sekta mkawasiliano ili tuweze kushirikiana kikamilifu katika kutambua viashiria vya uhamishaji wa miamala ya fedha ambayo sio ya kawaida na kutoa taarifa kwa mamlaka husika," amesema.

 Ofisa Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Dorolosa Maricky amesema wanashirikiana na TPSF kuwajengea uelewa zaidi wa namna gani ya kukabiliana na ujangili.

"Kama tunavyoelewa ujangili hautendeki kwa mtu mmoja au taasisi moja bali unakuwa na mnyororo, hivyo lazima tuwe na ushirikiano na taasisi mbalimbali ili kuweza kuzuia na kukata mnyororo wa ujangili.

"Miamala ya fedha inayofanywa kwa kujirudia kwenye maeneo ya maliasili ni ya kuijengea shaka na ndio maana tupo hapa kuwajengea uwezo wenzetu ili waweze kutusaidia kutupa taarifa zenye viashiria vya ujangili," amesema Maricky.

Amesema wa mafunzo hayo kwa sekta za fedha na mawasiliano itasaidia kama taasisi kuweza kuwa sehemu ya jitihada ya kupambana na ujangili.

Mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo, Esther Wangoi kutoka Tamno, amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafa kutokana na Serikali kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ujangili.

Mkurugenzi wa Utafiti na Uchechemuzi kutoka TBA, Tandasi Dan amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali, bado sekta binafsi, jamii na taasisi nyingine zinawajibu wa kuendeleza ushirikiana katika kukabiliana tatizo hilo.