Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMDA yateketeza dawa tani 35,000

Muktasari:

  • Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika kipindi cha 2021/22 imeteketeza dawa tani 35,547 zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

  


Dodoma. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika kipindi cha 2021/22 imeteketeza dawa tani 35,547 zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Imeelezwa kuwa kiasi hicho cha dawa kingepelekwa sokoni kilikuwa na thamani ya zaidi ya Sh35 bilioni na kwamba kingeweza kuleta madhara kwa binadamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 29, 2022 na Mkurugenzi wa TMDA, Adam Fimbo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu taarifa ya utekelezaji wa shughuli zao kwa mwaka 2021/22.

Fimbo amesema mbali na kuteketeza kiwango hicho wanaendelea kutoa elimu na kuwaajibisha watu wanaokiuka sheria ikiwamo kutoza faini.

Mkurugenzi huyo ametangaza kuongeza kasi kwa ajili ya kudhibiti dawa zisizofaa zisiingizwe sokoni ili kuendelea kulinda afya za Watanzania ambalo ni jukumu lao.

Amesema jumla ya dawa na vifaa tiba 8,831 vimesajiliwa nchini hadi sasa ambapo viwanda 17 vya dawa vimeruhusiwa na 17 ni vinavyotengeneza vifaa tiba huku 26 vikiwa ni viwanda vifaa tiba na 6 ni viwanda wa gesi tiba.

“Tunavyo jumla ya vituo vya forodha 32 ambavyo kwa baadhi ya maeneo vinafanya kazi saa 24 hasa katika Jiji la Dar e salaam, lengo letu ni kuendelea kuwa Mamlaka bora yenye udhibiti wa kusaidia jamii ya Watanzania,” amesema Fimbo.