Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TCU: Udahili vyuo vikuu waongezeka

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa

Muktasari:

  • Idadi ya waliodahiliwa yaongezeka huku nafasi za vyuo vikuu kudahili waombaji wa shahada ya kwanza zikiongezeka kwa asilimia 8.2 ikilinganishwa na mwaka wa masomo uliopita.

Dar es Salaam. Wanafunzi 86,624 sawa na asilimia 74.6 ya waliotuma maombi, wamechaguliwa kujiunga na vyuo vikuu 80 vilivyoidhinishwa kudaili wanafunzi wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Takwimu hizi ni za awamu ya kwanza ya udahili ambapo jumla ya maombi 116,133 yalitumwa na kuwezesha 86,624 kuchaguliwa.

Kati ya hao waombaji 43213 wamedahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja hivyo wametakiwa kujithibitisha kwenye chuo kimojawapo ili kuacha nafasi kwa wengine ambapo bado hawajapata udahili.

Akizungumza leo Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa, amesema kwa mwaka wa masomo 2023/2024; kuna nafasi 186,289 za wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Profesa Kihampa amebainisha kuwa ikilinganishwa na mwaka wa masomo uliopita, mwaka huu kuna ongezeko nafasi 14,121 sawa na asilimia 8.2.

Mbali na ongezeko hilo la waliodahiliwa katibu mtendaji huyo ameeleza kuwa kuna ongezeko la programu zilizotuhusiwa kudahili kwa mwaka mpya wa masomo kufikia 809 kutoka 757 za mwaka uliopita.

Kufungwa kwa awamu ya kwanza ya udahili kumetoa fursa ya kufunguliwa kwa awamu ya pili itakayoanza leo Agosti 25 ikitarajiwa kukamilika Septemba 6.