Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tarehe hukumu rufaa ya Sabaya kujulikana Machi 15

Muktasari:

  • Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesema Machi 15, 2022 itatoa tarehe ya hukumu ya rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kupinga kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

  

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesema Machi 15, 2022 itatoa tarehe ya hukumu ya rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kupinga kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 15, 2021 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hakimu Mwandamizi, Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu likiwamo la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 21, 2022 Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma amesema usikilizwaji wa shauri hilo umefika mwisho.

"Shauri lilipangwa kusikilizwa kwa muda maalumu na muda huo umemalizika. Shauri litakuja kwa ajili ya mention (kutajwa) Machi 15 na itajulikana uamuzi wa shauri hili utatolewa lini,” amesema Jaji

Katika kupinga rufaa hiyo mawakili wa Serikali wameeleza kuwa hati iliyowatia hatiani haikuwa batili kama wanavyodai mawakili wa Sabaya na wenzake na kwamba ilikidhi matakwa ya kisheria.

Wameitaka mahakama itupilie mbali rufaa hiyo kwani haina msingi kisheria.

Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja Oktoba 15, mwaka jana.

Kina Sabaya waliwakilishwa na jopo la mawakili sita likiongozwa na Majura Magafu, Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa, Sylvster Kahunduka, Edmund Ngemela na Fridolin Bwemelo ambao kwa pamoja wanaitaka mahakama iridhie hoja zao 14 za rufaa na iwaachie huru wateja.