Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yatarajia kubadilisha ikolojia ya kidijitali

Dar es Salaam. Serikali inatarajia kubadilisha ikolojia ya kidijitali na kukuza mapato ya ndani kupitia teknolojia ya mtandao wa Airtel Tanzania. Hivyo mtandao huo unatarajiwa kuziunga harakati za kubadilisha sekta ya kidijitali nchini kupitia kuwashwa kwa Kituo cha Mkongo wa Chini ya Bahari wa 2Africa kilichopo Mbezi, jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa miundombinu hiyo mipya ya mkongo wa mawasiliano wa chini ya Bahari utachangia kuinua na kubadilisha sekta ya kidijitali nchini kupitia mtandao wa intaneti ulioimara ambao kwa sasa unatumiwa na watu bilioni tatu duniani kote.

Akizungumza hayo katika Mkutano wa Connect 2 Connect wa mwaka 2024 uliofanyika Septemba 18, 2024 jijini Arusha, Mhandisi Mkuu wa Mtandao wa Airtel Tanzania, Dkt Adedoyin Adeola, ambae ni mmoja wa wachokoza mada katika mkutano huo ameeleza kuwa, Mkongo wa chini ya Bahari wa 2Afrika wenye urefu wa kilomita 45,000 ni tunu muhimu inayoenda kubadilisha ikolojia ya kidijitali nchini kwa kuwa italeta mchango mkubwa katika maendeleo ya kidijitali.

“2Afrika inatarajia kuleta miundombinu muhimu ya intaneti na kuunganisha watu takribani bilioni 1.2 na zaidi. Mkongo huu utaleta mabadiliko ya kipekee katika upatikanaji wa huduma za kidijitali barani Afrika, kuchochea ukuaji wa kiuchumi, kuongeza usawa na kuchangia katika ubunifu wa kiteknolojia.

Hii itaiweka Afrika katika nafasi nzuri ya kuunganishwa na uchumi wa kidijitali wa dunia ambao ni jumuishi, wezeshi na endelevu kwa ajili ya bara zima. Mkongo huu unaiweka Tanzania katika nafasi ya kuwa kitovu cha teknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki na barani Afrika,” Alisema Dk Adeola.

Pia ameongeza kuwa kituo cha Mkongo wa Bahari kitakuwa daraja litakaloziba ufa wa mgawanyiko wa kidijitali kati ya maeneo ya mijini na vijijini kwa kuboresha upatikanaji wa intaneti na kuendesha ukuaji wa biashara za mtandaoni, na kuchochea ongezeko la vyanzo vya mapato kwa serikali na ikiwamo kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Joseph Muhere amesema kuwa mtandao huo unaunga mkono safari ya mabadiliko kuelekea uchumi kamili wa kidijitali kupitia miundombinu ya hali ya juu ambayo iko sambamba na maono ya taifa ya kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi na kijamii Pamoja na ujumuishwaji wa kidijitali.